NEC Yaanzisha Mfumo wa Kupata Kitambulisho Online OVRS
NEC Yaanzisha Mfumo wa Kupata Kitambulisho Online OVRS
NEC Yaanzisha Mfumo wa Kupata Kitambulisho Online OVRS, NEC Yaanzisha Mfumo wa Kupata Kitambulisho Cha Mpiga Kura Mtandao, Jinsi ya Kujiandikisha Kupata Kitambulisho Cha Mpiga Kura Online, Online Voters Registration System (OVRS) Tanzania,Mfumo wa Uboreshaji wa Taarifa za Mpiga Kura Mtandaoni
MFUMO WA KUANZISHA MCHAKATO WA KUBORESHA TAARIFA ZA MPIGA KURA
Ndugu mpiga kura, anzisha mchakato wa awali wa kuboresha taarifa za mpiga kura kwa njia ya mtandao.
Baada ya kukamilisha hatua hii utapaswa kufika katika kituo cha kujiandikisha ndani ya kata husika kwaajili ya kumalizia mchakato na kupewa kadi ya Mpiga Kura.
Uboreshaji wa taarifa utahusisha kurekebisha au kubadili taarifa binafsi, kuhama kituo na kurekebisha au kubadili taarifa binafsi na kuhama kituo kwa kubonyeza kitufe husika.
MAELEKEZO YA KUREKEBISHA AU KUBADILI TAARIFA BINAFSI
Kurekebisha au kubadili taarifa binafsi, mpiga kura atapaswa kufanya yafuatayo:
- kujaza namba ya mpiga kura;
- kujaza mwaka wa kuzaliwa;
- kujaza namba ya kitambulisho cha Taifa (NIDA); na
- kujaza namba ya simu inayotumika kwa sasa.
Taarifa zitakazopatikana baada ya kujaza namba ya kitambulisho cha Taifa (NIDA) ndizo zitakazotumika kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
MAELEKEZO YA KUHAMA KITUO
Kuhamisha taarifa za Mpiga Kura kutoka eneo moja la kiuchaguzi kwenda eneo lingine, mpiga kura atapaswa kufanya yafuatayo: –
- kujaza namba ya mpiga kura ;
- kujaza mwaka wa kuzaliwa;
- kujaza namba ya simu inayotumika kwa sasa; na
- kuchagua kata anayotaka kuhamia.
- Mpiga kura atachagua kata anayotaka kuhamia na itampasa kufika kwenye kituo cha kata husika ili kukamilisha mchakato na kupewa kadi.
MAELEKEZO YA KUREKEBISHA AU KUBADILI TAARIFA BINAFSI NA KUHAMA KITUO
Kurekebisha au kubadili taarifa binafsi na kuhamisha taarifa kutoka kituo cha awali kwenda kituo kingine, mpiga kura anapaswa kufanya yafuatayo: –
- kujaza namba ya mpiga kura;
- kujaza mwaka wa kuzaliwa;
- kujaza namba ya kitambulisho cha Taifa (NIDA); na
- kujaza namba ya simu inayotumika kwa sasa.
Taarifa zitakazopatikana baada ya kujaza namba ya kitambulisho cha Taifa (NIDA) ndizo zitakazotumika kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
BORESHA TAARIFA ZA MPIGA KURA MTANDAONI
BONYEZA HAPA KUANZISHA MCHAKATO WA KUBORESHA TAARIFA ZA MPIGA KURA
Tags: Jinsi ya Kujiandikisha Kupata Kitambulisho Cha Mpiga Kura Online, Mfumo wa Uboreshaji wa Taarifa za Mpiga Kura Mtandaoni, NEC Yaanzisha Mfumo wa Kupata Kitambulisho Cha Mpiga Kura Mtandao, NEC Yaanzisha Mfumo wa Kupata Kitambulisho Online OVRS, Online Voters Registration System (OVRS) Tanzania
Sawa
Kitambulisho cha mpiga kura