SIMBA Wamgomea Chama Awashitaki TFF
SIMBA Wamgomea Chama Awashitaki TFF
SIMBA Wamgomea Chama Awashitaki TFF, Kiungo mpya wa Klabu ya Yanga, Clatous Chama amefungua shauri kwenye mamlaka ya soka nchini akidai kuwa waajiri wake wa zamani Simba SC hawajampa Release Letter ambayo itampa uhalali wa kuichezea Klabu ya Yanga.
Klabu ya Simba inaelezwa kuwa imekataa kumpa Release Letter ikidai aliondoka kinyume cha Utaratibu kwenda Yanga.
Shauri hilo limesikilizwa leo 16 Julai 2024 pamoja na lile la Lameck Lawi mchezaji wa Coastal Union msimu wa 2023/2024.
Lawi alitambulishwa na Simba akiwa Mchezaji wa kwanza Klabu hiyo ikifanya Maboresho makubwa ya Kikosi chake kuelekea Msimu Mpya wa 2024/2025.
Baada ya kutambulishwa Simba, uongozi wa Coastal Union ulibainisha kuwa bado mchezaji huyo ni mali yao kwani Simba walienda kinyume na Makubaliano.