TFF Yafanya Maboresho ya Kanuni za Ligi 2024
TFF Yafanya Maboresho ya Kanuni za Ligi 2024
TFF Yafanya Maboresho ya Kanuni za Ligi 2024, Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) katika kikao chake cha Agosti 1, 2024 ilijadili na kufanyia maamuzi maoni ya maboresho ya Kanuni za Ligi kwa ajili ya toleo la 2024.
Kanuni zilizofanyiwa maboresho na kupitishwa katika kikao hicho ni pamoja na Kanuni ya 7 ya First League kuhusu Nane Bora na Kanuni 7 (saba) za Ligi Kuu ambazo ni Kanuni ya 9 kuhusu uwanja, Kanuni ya 17 kuhusu Taratibu za Mchezo, Kanuni ya 31 kuhusu Kutofika Uwanjani, Kanuni ya 47 kuhusu Udhibiti kwa Klabu, Kanuni ya 62 kuhusu Wachezaji wa kigeni, Kanuni ya 77 kuhusu Makocha na Kanuni ya 79 kuhusu Maamuzi Yasiyokatiwa Rufaa.
Aidha kamati hiyo ilipitisha kanuni mpya 12 ambazo zitajumuishwa kwenye toleo la 2024.
Maboresho yote ya Kanuni za Ligi Kuu 2024 yataathiri Kanuni za mashindano mengine yaliyo chini ya TFF na machapisho yake yatatangazwa.
Unaweza Kudownload Maboresho yote kwenye PDF hapa chini;