UBORESHAJI wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Kudumu hadi Aprili 2025
UBORESHAJI wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Kudumu hadi Aprili 2025
UBORESHAJI wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Kudumu hadi Aprili 2025, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imesema kuwa kazi ya uboreshaji wa Daftari Ia Kudumu la Wapiga Kura itafikia tamati Aprili mwakani, huku wakazi wa Dar es Salaam wakianza kuandikishwa Machi, mwakani.
Uandikishaji huo tayari umezinduliwa Julai 20, 2024 Mkoani Kigoma Kutoka Julai Mosi iliyopangwa awali, kabla ya INEC kutangaza Mabadiliko.
Uboreshaji awamu ya Kwanza umeanzia kwenye mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora, huku awamu ya pili ikiwa ni mikoa ya Kagera na Geita.
Kailima amesema kuwa awamu ya tatu itakuwa kwenye mikoa ya Shinyanga na Mwanza na ya nne ni Mikoa ya ya Simiyu na Mara na baadhi ya Halmashauri za Mkoa wa Manyara.
“Tutakwenda hivyo hadi tutakapomaliza, mwanzo tulipanga tufikie tamati Machi mwakani, lakini sasa tutafikia tamati Aprili na Dar es Salaam imepangwa peke yake kutokana na changamoto zake na uandikishaji wake utakuwa ni Machi mwakani,” amesema Kailima.
Tags: UBORESHAJI wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Kudumu hadi Aprili 2025