USAJILI Awesu Awesu ni Mnyama
USAJILI Awesu Awesu ni Mnyama
USAJILI Awesu Awesu ni Mnyama, Klabu ya Simba SC imekamilisha usajili wa Kiungo mshambuliaji, Awesu Awesu kutoka KMC FC kwa mkataba wa miaka miwili.
Awesu amejiunga na Simba kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na KMC aliyodumu nayo kwa miaka mitatu.
Pia Awesu ni mchezaji mzoefu kwenye Ligi Kuu ya NBC na anaweza kumudu nafasi ya kiungo wa Ushambuliaji na winga zote ingawa pia amewahi kutumika kama kiungo mkabaji.
Mbali na KMC, Awesu amewahi kuzitimikia timu za Kagera Sugar, Azam FC na Mwadui FC kwa nyakati tofauti.
Awesu Awesu anakuwa Mchezaji wa 14 kusajiliwa na Simba kuelekea msimu ujao wa Ligi wa 2024/2025 baada ya kukamilisha usajili wa Wachezaji wengine ambao ni;
Kelvin Kijili kutoka Singida Fountain Gate, Yusuph Kagoma Kutoka Singida Fountain Gate, Karaboue Chamou Kutoka Racing Club d’ Abidjan ya Ivory Coast, Valentin Nouma kutoka St. Eloi Lupopo ya DR Congo, Omary Omary Kutoka Mashujaa FC, Debora Fernandes Mavambo Kutoka Mutondo Stars ya Zambia, Augustine Okejepha Kutoka Rivers United ya Nigeria na Valentino Mashaka Kutoka Geita Gold FC.
Wengine ni Abdulrazack Mohamed Hamza kutoka Super Sport ya Afrika Kusini, Lameck Lawi kutoka Coastal Union, Joshua Mutale kutoka Power Dynamos, Steven Mukwala kutoka Asante Kotoko na Jean Charles Ahoua kutoka Stella Club d’Adjamé.