USAJILI Kelvin Kijili ni Mnyama
USAJILI Kelvin Kijili ni Mnyama
USAJILI Kelvin Kijili ni Mnyama, Klabu ya Simba SC imekamilisha usajili wa mlinzi wa kulia, Kelvin Kijili kutoka Singida Fountain Gate kwa mkataba wa miaka miwili.
Kijili mwenye umri wa miaka 24 ni kijana mwenye kipaji na kasi amekuwa akitumika kuanzisha mashambulizi kutokea upande wa kulia.
Akiwa na Singida Fountain Gate msimu uliopita Kijili amesaidia kupatikana kwa mabao manne (assist).
Aidh Usajili uliofanyika na Simba kuelekea msimu mpya wa mashindano umezingatia kigezo cha umri kwakuwa malengo ya Klabu hiyo ni kujenga timu imara ya muda mrefu.
Kijili tayari amejiunga na Wachezaji wenzake kambini nchini Misri kuendelea na maandalizi ya msimu mpya wa mashindano 2024/2025.
Kelvin Kijili anakuwa Mchezaji wa 13 kusajiliwa na Simba kuelekea msimu ujao wa Ligi wa 2024/2025 baada ya kukamilisha usajili wa Wachezaji wengine ambao ni;
Yusuph Kagoma Kutoka Singida Fountain Gate, Karaboue Chamou Kutoka Racing Club d’ Abidjan ya Ivory Coast, Valentin Nouma kutoka St. Eloi Lupopo ya DR Congo, Omary Omary Kutoka Mashujaa FC, Debora Fernandes Mavambo Kutoka Mutondo Stars ya Zambia, Augustine Okejepha Kutoka Rivers United ya Nigeria na Valentino Mashaka Kutoka Geita Gold FC.
Wengine ni Abdulrazack Mohamed Hamza kutoka Super Sport ya Afrika Kusini, Lameck Lawi kutoka Coastal Union, Joshua Mutale kutoka Power Dynamos, Steven Mukwala kutoka Asante Kotoko na Jean Charles Ahoua kutoka Stella Club d’Adjamé.