WALIMU 54000 Kupandishwa Madaraja kwa Mseleleko
WALIMU 54000 Kupandishwa Madaraja kwa Mseleleko
WALIMU 54000 Kupandishwa Madaraja kwa Mseleleko, Jumla ya walimu 54,000 nchini ambao waliachwa nyuma kimadaraja wanatarajia kupandishwa madaraja yao ifikapo mwezi julai 2024 ili kuleta usawa wa madaraja kwa kuzingatia kiwango cha Elimu na muda wa Ajira.
Hayo yamebainishwa tarehe 3 Juni 2024 na Afisa Elimu Mkoa wa Dodoma Vicent Kayombo akimwakilisha Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- TAMISEMI Mkoani Ruvuma.
Akizungumza na Walimu Wakuu, Wakuu wa Shule, Maafisa Elimu Kata pamoja na walimu wa Wilaya ya Mbinga, Kayombo amesema
WALIMU 54000 Kupandishwa Madaraja kwa Mseleleko
“Katibu Mkuu TAMISEMI amenituma nije niwaambie kwanza Serikali inatujali sana sisi walimu haijatusahau inataka walimu wote wawe kwenye hali sawa ikilinganishwa na kiwango cha elimu na madaraja yao”
Wakati Serikali ikiendelea kuboresha Sekta ya Elimu nchini Kayombo amesema Katibu Mkuu OR-TAMISEMI anawataka Walimu hao kutimiza majukumu yao ya kusimamia malezi ya wanafunzi pamoja na kuhakikisha wanafunzi wote wanapata umahiri badala ya kuwakatia tamaa.
“Kuna baadhi ya Walimu wenzetu hawatimizi majukumu yao wengine wanadiriki hata kuwaambia wanafunzi hili somo la sayansi ni gumu hakuna somo gumu tuache huo ushamba fikiria angekuwa mwanao ungefanyaje” Amesema Kayomboll
Sambamba na hilo amewataka Wakuu wa Shule pamoja na Walimu Wakuu kuimarisha Ushirikiano na Walimu ili kurahisisha Utendaji kazi na Kuboresha Ujifunzaji na Ufundishaji.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Maurus Hyera amebainisha kuwa maagizo yote ambayo yametolewa na Katibu Mkuu OR-TAMISEMI yatatekelezwa ili kuendelea kuleta mageuzi katika Sekta ya Elimu nchini.
Madaraja mserereko 2024