YANGA Bingwa CRDB Bank Federation Cup 2024
YANGA Bingwa CRDB Bank Federation Cup 2024
YANGA Bingwa CRDB Bank Federation Cup 2024,Klabu ya Young Africans imefanikiwa kutwaa Kombe la Shirikisho la Tanzania (TFF), Maarufu CRDB Bank Federation Cup baada ya ushindi wa penaltı 6-5 dhidi ya Azam FC kufuatia sare ya bila mabao ndani ya dakika 120.
Mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, ulishuudiwa penati za Yanga zikifungwa na Pacome Zouzoua, Kouassi Attohoula Yao, Bakari Mwamnyeto, Khalid Aucho, Kennedy Musonda na Jonas Mkude.
Kwa upande wa Azam FC ni penati zilifungwa na Adolph Mutasingwa Bitebeko, Cheikh Sidibé, Kipré Junior, Edward Charles Manyama na Feisal Salum Abdallah.
Waliokosa Kwa Yanga ni Stephane Aziz Ki, Joseph Guerde hawa mikwaju yao iliokolewa na kipa wa Azam FC, Mohamed Mustafa huku İbrahim Abdallah akipaisha juu.
Waliokosa kwa Azam FC ni Yeison Fuentes Mendoza huyu aligongesha mwamba, Gibril Silah na Lusajo Mwaikenda wao mikwaju yao iliokolewa na Kipa Djigui Diarra huku Iddi Suleiman akipaisha juu ya lango.
Hiyo ilikuwa ni Fainali ya tisa tangu kurejea kwa Michuano hiyo msimu wa 2015/2016 na hilo ni taji la tatu mfululizo, huku kikiwa kipigo cha tatu cha Fainali kwa Azam mbele ya Yanga.
Pia ulikuwa Mchezo wa pili wa Fainali za Michuano hiyo kuamuliwa kwa penati baada ya ile ya msimu wa 2021-2022 ambapo Yanga iliifunga Coastal Union kwa penati 3-2 baada ya dakika 120 kuisha kwa sare ya 3-3.
Katika hatua nyingine, Ibrahim Abdallah alichaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Fainali hiyo na kuvuna Sh 1 milioni, huku Clement Mzize akitangazwa Mfungaji Bora akifunga matano sawa na aliyomalizana nayo Edward Songo wa JKT Tanzania.
Hilo linakuwa taji la nne kwa Yanga tangu Michuano hiyo iliporejeshwa, lakini ni la nane kwa jumla tangu michuano ilipoasisiwa ikiwa na jina la Kombe la FAT mwaka 1967 kisha kuwa Kombe la FA lililozimikwa rasmi mwaka 2002.