RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


JINSI ya Kujisajili NIDA eonline.nida.go.tz

Filed in Ajira, Makala by on 15/07/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

JINSI ya Kujisajili NIDA eonline.nida.go.tz

JINSI ya Kujisajili NIDA eonline.nida.go.tz, JINSI ya Kujisajili NIDA Online, Mfumo wa maombi ya Kitambulisho cha Taifa, Mfumo wa maombi ya Kitambulisho cha Taifa NIDA, Mfumo wa maombi ya Kitambulisho cha NIDA, Mfumo wa maombi ya Kitambulisho cha NIDA Mtandaoni, Mfumo wa maombi ya Kitambulisho cha NIDA Online.

JINSI ya Kujisajili NIDA eonline.nida.go.tz

JINSI ya Kujisajili NIDA eonline.nida.go.tz, JINSI ya Kujisajili NIDA Online, Mfumo wa maombi ya Kitambulisho cha Taifa, Mfumo wa maombi ya Kitambulisho cha Taifa NIDA, Mfumo wa maombi ya Kitambulisho cha NIDA, Mfumo wa maombi ya Kitambulisho cha NIDA Mtandaoni, Mfumo wa maombi ya Kitambulisho cha NIDA Online.

MFUMO WA MAOMBI YA KITAMBULISHO CHA TAIFA NIDA.

Hii ni huduma inayomuwezesha mwombaji wa kitambulisho cha Taifa (Raia au Mgeni mkazi) kujaza fomu ya maombi ya Kitambulisho cha Taifa kwa njia ya Kielektroniki akiwa mahali popote.

Baada ya kujaza fomu hiyo, mwombaji atatakiwa kuichapisha (Print) na kuiwasilisha pamoja na vielelezo vingine katika Ofisi ya NIDA (wilaya) iliyo karibu naye kwaajili ya kukamilisha usajili wa alama za biometria.

VIELELEZO VYA LAZIMA KWA RAIA VINAVYOHITAJIKA WAKATI WA UOMBAJI WA KITAMBULISHO CHA TAIFA

  • Cheti cha kuzaliwa cha mwombaji
    Nakala ya cheti cha kuzaliwa / kiapo cha mzazi mmoja.
  • Kama uraia wa mwombaji ni wakurithi: thibitisha kwa nakala ya cheti cha kuzaliwa au nakala ya kitambulisho cha Taifa cha mzazi mmoja.
  • Kama uraia wa mwombaji ni wa kujiandikisha, thibitisha kwa nakala ya uraia wa kujiandikisha (Dossier Number) ya mwombaji.

KUJISAJILI BONYEZA HAPA

KULOGIN/KUINGIA BONYEZA HAPA

Mambo Muhimu ya kuzingatia wakati wa Ujazaji Fomu

  • Mwombaji anatakiwa kuwa na anuani ya barua pepe ambayo ataitumia kujisajili na kupokea kiunga kitakachomuwezesha kukamilisha usajili wake.
  • Mwombaji anatakiwa kuwa na nyaraka zisizopungua mbili zitakazotumika kuthibitisha utambulisho wake. Mfano wa nyaraka hizo ni; Cheti cha kuzaliwa n.k.
  • Mwombaji anatakiwa kufanya “scanning” ya nyaraka zake na kuziweka katika muundo wa PDF (usiozidi kurasa moja kwa kila kiambatisho) au picha katika muundo wa JPG au PNG.
  • Ni muhimu Mwombaji kujaza Namba yake ya simu ya mkononi.
  • Mwombaji anatakiwa kuambatisha cheti cha kuzaliwa endapo amezaliwa Mwaka 1980 na kuendelea. Aidha, endapo Mwombaji amezaliwa kabla ya mwaka 1980 anatakiwa kuambatisha cheti cha kuzaliwa au “Affidavit”.
  • Kwa Waombaji wenye majina mengine; ni vyema kuandika majina hayo ili endapo ikatokea uhitaji wa kurekebisha majina yake iwe rahisi kutambulika.
  • Mwombaji anatakiwa kufahamu majina ya Baba na Mama yake mzazi.
  • Mwombaji ambaye ana Namba za Utambulisho (NIN) za wazazi wake; anatakiwa kuweka viambata halisi (kwa wazazi waliokwishapata vitambulisho vya Taifa).
  • Mwombaji anatakiwa kujua namba ya Nyumba, Mtaa na kata anayoishi.
  • Kwa Watanzania walioko nje ya Nchi, wanatakiwa kupata uthibitisho wa ukaazi katika Nchi husika kutoka kwa Afisa wa Ubalozi wa Tanzania ili kujaza sehemu ya makazi, Mtaa/Kata kwa usahihi.
  • Endapo Mwombaji amepata vyeti vya Shule, Namba ya mlipa kodi (TIN) na Kadi ya mpiga kura; ni vyema kuambatanisha.
  • Mwombaji anatakiwa kujaza Fomu kwa usahihi na kuhakikisha viambata vyake na taarifa alizo jaza katika mfumo hazikinzani na taarifa nyingine, kama vile taarifa za Shule au Biashara.
  • Mwombaji anatakiwa kujaza taarifa zake kwa usahihi, na kuchapisha taarifa hizo katika fomu na kwenda kwenye Ofisi ya Serikali ya Mtaa napoishi kwaajili ya kugongewa Mhuri na Saini ya Mwenyekiti wa Mtaa wake.
  • Mwombaji anatakiwa kufika katika Ofisi ya NIDA iliyoko kwenye Wilaya yake ya makazi akiwa na fomu iliyokamilika (Fomu iliyogongwa Mhuri na kuwekwa Saini ya Mwenyekiti wa Serikali wa Mtaa), pamoja na nakala ngumu za viambatisho vyake alivyopakia katika mfumo wakati wa usajili kwaajili ya kukamilisha taratibu za usajili.
  • Kwa Mwombaji ambaye anahitaji kupata maelezo ya ziada; asisite kufika katika ofisi ya NIDA iliyopo karibu.

ENDELEA NA USAJILI 

MAWASILIANO MAKAO MAKUU

  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  •  12324 Dar Es Salaam,
  •  *255 735 201 020
  •  info@nida.go.tz
  •   

HUDUMA KWA MTEJA

  • 0752 000 058
  • 0687 088 888
  • 0777 740 006
  • 0677 146 666

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags: , , , , , ,

Comments are closed.