RASMI Ligi Kuu ya NBC 2023/2024 Yatamatika
RASMI Ligi Kuu ya NBC 2023/2024 Yatamatika
RASMI Ligi Kuu ya NBC 2023/2024 Yatamatika, Msimu wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara 2023/2024 umehitimishwa kwa Azam FC kumaliza nafasi ya pili nyuma ya mabingwa, Yanga huku Simba SC wakimaliza nafasi ya tatu na Coastal Union nafasi ya nne.
Azam FC imemaliza nafasi ya pili baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya JKT Tanzania, licha ya ushindi wa 2-0 pia dhidi ya JKT Tanzania Simba imemaliza nafasi ya Tatu ilipokuwa.
Azam imemaliza na pointi 69 sawa na Simba ikiizidi tu wastani wa mabao wote wakiwa nyuma ya Yanga iliyomaliza na pointi 80 baada ya ushindi wa 4-1 dhidi ya Tanzania Prisons.
Bingwa wa Ligi Kuu na mshindi wa pili wamefuzu Ligi ya Mabingwa Afrika na mshindi wa tatu na wa nne wamefuzu kucheza Kombe la Shirikisho Afrika 20204/2025.
Aidha, Kiungo Mshambuliaji Stephane Aziz Ki ameibuka Mfungaji Bora kwa baadae ya kupata mabao 21 mbele ya Feisal Salum Abdallah wa Azam FC aliyefunga mabao 19.
Mechi nyingine za Ligi Kuu kwa mechi za mwisho wa Msimu, Coastal Union imetoka sare ya bila mabao na KMC.
Namungo imeichapa 3 – 2 Tabora United, Mashujaa FC imeichapa Dodoma Jiji 3 – 0, Ihefu SC imeichapa 5 – 1 Mtibwa Sugar na Kagera Sugar imeichapa, Singida Fountain Gate 3-2.
Kwa matokeo hayo, Mtibwa Sugar ya Morogoro na Geita Gold ya Geita zimeshuka Daraja hadi Ligi Daraja la Kwanza (Championship) msimu wa 2024/2025, huku Tabora United na JKT Tanzania zikiangukia Play-Off kuwania kubaki Ligi Kuu.
Timu hizo zitacheza mechi mbili nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atasalia Ligi Kuu na takayepoteza atakwenda kucheza na Biashara United iliyofuzu kutoka Championship kuwania kurudi Ligi Kuu.