VIWANGO Vya Mishahara ya Watumishi 2024
VIWANGO Vya Mishahara ya Watumishi 2024
VIWANGO Vya Mishahara ya Watumishi 2024,Viwango vya Mishahara ya Watumishi wa UMMA Mwaka 2024, Viwango vya Mshahara kwa Watumishi wa Umma Tanzania 2024,Viwango vipya Mishahara serikalini 2024/2025, Salary Scale Tanzania 2024/2025,Nafasi za kazi wizara ya elimu 2024.
Serikali inaendelea kutekeleza Sera ya malipo ya Mshahara na Motisha katika Utumishi wa Umma ya Mwaka 2010.
Katika hatua za kutimiza malengo ya Sera hii, Serikali imefanya marekebisho ya mishahara ya watumishi wake kuanzia tarehe 1 Julai, 2022.
Kufuatia marekebisho hayo, kima cha chini cha mshahara kimeongezwa kwa asilimia 23.3 kutoka shlingi 300,000 kwa mwezi hadi shilingi 370,000 kwa mwezi.
Ngazi nyingine za mshahara zimeongezwa kwa asilimia tofauti.
Kutokana na mabadiliko haya, upeo wa ngazi za mishahara iliyotolewa kwa Waraka wa Watumishi wa Serikali Na. 1 wa mwaka 2015, sasa utakuwa kama ilivyooneshwa katika Viambatanisho Na. 1 11 vya Waraka huu.
Aidha, vianzia mshahara kwa msingi wa Elimu, Muda wa Mafunzo, aina ya kazi na ujuzi vitakuwa kama vilivyoainishwa katika Miundo ya Maendeleo ya Utumishi ya kada husika pamoja na miongozo mbalimbali iliyotolewa na Ofisi hii.
Wanaohusika na Marekebisho haya ya mshahara
Marekebisho haya yanawahusu watumishi wa Serikali Kuu, Watumishi wa Serikali za Mitaa, Watumishi walioshikizwa kwenye Taasisi za Umma pamoja na Watumishi ambao watakuwa kwenye likizo inayoambatanana na kuacha kazi au kustaafu kazi baada ya tarehe 1 Julai, 2022.
Watumishi Wanaopata Mishahara Binafsi
Watumishi ambao wanapata Mishahara binafsi (Personal Salaries) iliyo ndani ya viwango vya mishahara ya Serikali na ambayo ni mikubwa kuliko ile ya vyeo vyao halisi (Substantive Post) Serikalini, watahusika na marekebisho haya iwapo vyeo na mishahara yao itaangukia katika vyeo na ngazi mpya za mishahara.
Aidha, Watumishi wanaopata Mishahara binafsi isiyo ndani ya viwango vya mishahara ya Serikali hawatahusika na marekebisho haya.
Tarehe ya Mabadiliko
Waraka huu utaanza kutumika tarehe 1 Julai, 2022 na unafuta Waraka wa Watumishi wa Serikali Na. 1 wa Mwaka 2015.
Waajiri wote wanaohusika na Waraka huu wanatakiwa kurekebisha mishahara ya Watumishi wao kulingana na viwango vilivyotolewa katika Waraka huu.
Waraka huu ni kumbukumbu na taarifa ya Serikali na hairuhusiwi kutangazwa kwenye vyombo vya habari.
Viwango vya Mshahara kwa Watumishi wa Umma nchini Tanzania kwa Mwaka 2024 ni kama ilivyoainishwa hapa chini;
TGOS A: Ranges from Sh240,000 (TGOS A 1) to Sh335,200 (TGOS A 18).
TGOS B: Starts at Sh347,000 (TGOS B 1) and goes up to Sh451,500 (TGOS B 12).
TGOS C: Begins at Sh471,000 (TGOS C 1) and ends at Sh592,000 (TGOS C 12).
TGS A: Ranges from Sh249,000 (TGS A 1) to Sh295,200 (TGS A 8).
TGS B: Starts at Sh311,000 (TGS B 1) and goes up to Sh387,500 (TGS B 10).
TGS C: Begins at Sh410,000 (TGS C 1) and ends at Sh520,000 (TGS C 12).
TGS D: Ranges from Sh567,000 (TGS D 1) to Sh693,500 (TGS D 12).
TGS E: Starts at Sh751,000 (TGS E 1) and goes up to Sh844,000 (TGS E 8).
VIWANGO VYA MISHAHARA YA WATUMISHI SERIKALINI DOWNLOAD PDF
Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ambayo Kitaifa yalifanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Mkoani Arusha tarehe 01 May 2024, alisema kuwa Serikali itaendelea kuhuisha viwango vya mshahara kwa kuzingatia uwezo wa kiuchumi na kibajeti pamoja na ujuzi na utendaji wa waajiriwa ili kuepuka kuchochea mfumuko wa bei, kuhatarisha uhimilivu wa deni la Taifa na athari nyingine kwenye utulivu wa uchumi wa Taifa kwa ujumla.
Alisema kuwa changamoto mbalimbali ambazo zimeikumba Dunia ikiwemo vita na majanga ya asili zimeendela kuathiri uchumi wa Taifa kutokana na kuvurugika kwa mfumo wa ugavi na kupanda kwa bei za mafuta, mbolea, chuma na chakula.
Mpango alisema luwa Pamoja na changamoto hizo tathmini ya Serikali na ya Taasisi za kimataifa ikiwemo IMF, Benki ya Dunia, AfDB, Moody’s, Fitch na zinginezo zimeonesha kuwa uchumi wa Taifa umekuwa stahimilivu kwa kiasi cha kuridhisha hivyo hali hiyo itakapoendelea kudumu wafanyakazi wawe tayari kunufaika.
Aidha alisema kuwa Serikali imeendelea kuboresha maslahi ya watumishi kwa namna mbalimbali, ikiwemo kwa kulipa nyongeza ya mwaka ya mshahara ambapo Mwaka 2023/24 kiasi cha shilingi bilioni 153.9 kililipwa na kwa mwaka 2024/25, Serikali imetenga shilingi bilioni 150.8 kwaajili hiyo.
Pia alisema Serikali imeendelea kuwapandisha vyeo watumishi mbalimbali, ambapo Mwaka 2023/24 jumla ya watumishi 81,515 walipandishwa vyeo na mwaka 2024/25 Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 252.7 kwaajili ya kuwapandisha vyeo Watumishi 219,924.
Makamu wa Rais aliongeza kuwa Serikali inathamini na kupokea hoja ya kuboresha Kanuni ya ukokotoaji wa mafao ambapo suala hilo ambalo ni la sayansi ya Watakwimu-bima litashauriwa kwa kuzingatia uhimilivu na uendelevu wa mifuko ya hifadhi ya jamii.
Halikadhalika Makamu wa Rais alisema likizo ya uzazi ni haki ya Mfanyakazi na iwapo mfanyakazi atajifungua mtoto au watoto njiti, kipindi cha uangalizi maalumu hakitahesabiwa kama likizo ya uzazi.
Alisema vilevile mfanyakazi husika ataruhusiwa kutoka kazini saa 7:30 kila siku kwa muda wa miezi sita baada ya kumalizika kwa likizo ya uzazi ili kumpa fursa ya kwenda kunyonyesha.
Aidha alisema Serikali ipo katika hatua ya kuifanyia marekebisho Sheria ya Ajira na Uhusiano Kazini, Sura 366 ili likizo ya uzazi ianze pale mtoto atakapomaliza kipindi cha uangalizi maalum kadri madaktari watakavyothibitisha.
Makamu wa Rais alitoa wito kwa wafanyakazi nchini kuendelea kutekeleza majukumu kwa bidii, maarifa, uadilifu kwa kutanguliza maslahi ya Taifa mbele kwa kuongeza tija katika utendaji kazi.
Alivisihi vyama vya wafanyakazi kushirikiana na Serikali na Waajiri kuhakikisha tija inaongezwa kwenye maeneo ya kazi kwa manufaa ya Taifa na wafanyakazi wenyewe.
Aidha aliwaasa wafanyakazi kuwa mstari wa mbele katika kudai risiti kila wanaponunua bidhaa na kuhakikisha risiti wanazopewa zimeandikwa gharama halisi ili kuiwezesha Serikali kupata mapato zaidi na kupelekea wigo mpana zaidi wa kuboresha maslahi ya wafanyakazi.
Maadhimisho ya Mei Mosi kitaifa yalihuduhuriwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Dotto Biteko, Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Deogratius Ndejembi, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Dkt. Moses Kusiluka, Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA) Tumaini Nyamhokya, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda, Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi John Mongela, Viongozi mbalimbali wa Serikali, Dini, Mahakama, Vyama vya Wafanyakazi pamoja na wafanyakazi sekta binafsi na serikali.
Tags: Nafasi za kazi wizara ya elimu 2024., Salary Scale Tanzania 2024/2025, Viwango vipya Mishahara serikalini 2024/2025, VIWANGO Vya Mishahara ya Watumishi 2024, Viwango vya Mishahara ya Watumishi wa UMMA Mwaka 2024, Viwango vya Mshahara kwa Watumishi wa Umma Tanzania 2024