RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


WALIOCHAGULIWA Kidato cha Tano Zanzibar 2024

Filed in Ajira, Michezo, NECTA by on 04/06/2024

WALIOCHAGULIWA Kidato cha Tano Zanzibar 2024

WALIOCHAGULIWA Kidato cha Tano Zanzibar 2024,MOEVT Zanzibar Waliochaguliwa kidato cha tano 2024, Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato Cha Tano Zanzibar 2024, Orodha ya Majina ya Waliopangiwa Kujiunga na Kidato Cha Tano na Chuo Chuo cha Sayansi cha Karume 2024, Zanzibar allocation system Form Five Selection 2024, Majina ya Wanafunzi waliochaguliwa kidato cha tano 2024 PDF,Zanzibar secondary advanced allocation system form five selection 2024, Zanzibar secondary advanced allocation system pdf, Zanzibar advance allocation system, Zanzibar Secondary advanced allocation system.

WALIOCHAGULIWA Kidato cha Tano Zanzibar 2024

WALIOCHAGULIWA Kidato cha Tano Zanzibar 2024,MOEVT Zanzibar Waliochaguliwa kidato cha tano 2024, Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato Cha Tano Zanzibar 2024, Orodha ya Majina ya Waliopangiwa Kujiunga na Kidato Cha Tano na Chuo Chuo cha Sayansi cha Karume 2024.

Wanafunzi 5,818 wamechaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha Tano Visiwani Zanzibar.

Idadi hiyo ya Wanafunzi imeongezeka kutoka 4,415 mwaka 2023 hadi kufikia 5,818 mwaka 2024 sawa na asilimia 21. Kati ya hao Wasichana ni 3,352 na Wavulana ni 2,466.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Jumanne Juni 4, 2024, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Ali Abdugulam Hussein amesema kati ya wanafunzi hao, waliotoka shule binafsi na kutimiza Sifa za kujiunga kidato cha Tano ni 1,070.

“Idadi kamili ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano mwaka 2024 ni 5,818, ambapo wa shule za Serikali ni 4,645 na kutoka shule binafsi ni 1,070 na watahiniwa wa kujitegemea ni 103,” alisema Naibu Waziri Abdugulam.

WANAFUNZI WATAKAOINGIA KIDATO CHA TANO 2024/2025 ZANZIBAR BONYEZA HAPA KUTAZAMA

Amesema wanafunzi hao wamegawanywa katika tahasusi za Masomo ya sayansi wakiwa 3,485, Sanaa 1,955, Uchumi na Biashara 200, Kompyuta 63 na Wanafunzi watakaoendelea na Masomo yao katika Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Karume (KIST) kwa Masomo ya Ufundi ni 115.

Kutokana na idadi ya wanafunzi kuongezeka, amesema wizara imeongeza shule sita, ili asiwepo Mwanafunzi atakayekosa nafasi.

Majina ya wanafunzi hao amesema yanapatikana kupitia tovuti ya wizara (website ya WEMA) www.moez.go.tz

Amesema wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano wanatakiwa kuripoti shuleni Julai mosi, 2024 kuanza Masomo na kwamba Maelezo zaidi kuhusu kanuni na sheria za shule zitatolewa na na Uongozi wa shule.

Kwa wanaotakiwa kuripoti Chuo cha Sayansi cha Karume, amesema watatakiwa kuripoti Oktoba, 2024 na maelekezo zaidi watapata wakifika chuoni.

BONYEZA HAPA KUTAZAMA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2024 ZANZIBAR

Form Five Selection Zanzibar 2024-2025

Tags: , , , , , , , , ,

Comments are closed.