EWURA Bei Mpya za Mafuta Tanzania July 03-2024
EWURA Bei Mpya za Mafuta Tanzania July 03-2024
EWURA Bei Mpya za Mafuta Tanzania July 03-2024,EWURA Bei Mpya ya Mafuta Kuanzia July 03-2024, EWURA New Fuel Price Tanzania July 2024, New Fuel Price Tanzania July 5-2024,Energy and Water Utilities Regulatory Authority, Bei Kikomo za Bidhaa za Mafuta ya Petroli kuanzia Jumatano tarehe 03-07-2024.
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU BEI KIKOMO ZA BIDHAA ZA MAFUTA YA
PETROLI KUANZIA JUMATANO, TAREHE 3 JULAI 2024
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), inatangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini zilizoanza kutumika kuanzia Jumatano ya tarehe 3 Julai 2024 saa 6:01 usiku.
Kwa mwezi Julai 2024, bei za rejareja na za jumla katika Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara ni kama zinavyoonekana katika Jedwali Na. 1 na 2, mtawalia.
JEDWALI 1: BEI KIKOMO ZA REJAREJA (SHILINGI/LITA)
Bei za mafuta za rejareja kwa maeneo mbalimbali ya miji, wilaya na mikoa ni kama zinavyooneshwa katika Jedwali Na. 3.
Mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi Julai 2024 yamechangiwa na kupungua kwa bei za mafuta yaliyosafishwa katika soko la dunia (FOB) kwa wastani wa asilimia 5.92 kwa mafuta ya petroli na asilimia 0.65 kwa mafuta ya dizeli; kuongezeka kwa wastani wa gharama za kubadilisha fedha za kigeni (applicable exchange rate) kwa asilimia 0.6; kuongezeka kwa gharama za uagizaji wa mafuta (premiums) kwa wastani wa
asilimia 1.60 kwa petroli na asilimia 3.35 kwa dizeli katika Bandari ya Dar es Salaam; kupungua kwa gharama za uagizaji wa mafuta kwa wastani wa asilimia 11.75 kwa petroli na asilimia 11.75 kwa dizeli katika Bandari ya Tanga; na kuongezeka kwag harama za uagizaji wa mafuta kwa wastani wa asilimia 11.25 kwa mafuta ya petrolin a asilimia 11.22 kwa mafuta ya dizeli katika Bandari ya Mtwara.
W lafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa rejareja wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei zinazooneshwa katika Jedwali Na. 3.
Aidha, wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa jumla wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei zinazooneshwa katika Jedwali Na. 2.
Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mfanyabiashara yoyote atakayekiuka AGIZO hili.
EWURA inapenda kuwakumbusha wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa jumla na rejareja pamoja na jamii kuzingatia yafuatayo: –
- a) bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli kwa eneo husika zinapatikana kupitia simu za mkononi kwa kupiga namba *152*00# na kisha kufuata maelekezo.
Huduma hii ni bure na inapatikana kupitia mitandao yote ya simu za mkononi hapa nchini. - b) Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2015, kifungu namba 166, bei za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko. EWURA itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa
za mafuta. - c) Kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani isipokuwa bei hizo zisizidi bei kikomo (Price cap) au kuwa chini ya bei iliyoruhusiwa (Floor Price) kama zilivyokokotolewa kwa mujibu wa
Kanuni za EWURA za Kupanga Bei za Mafuta za Mwaka 2022 zilizotangazwa tarehe 28 Januari 2022 kupitia Gazeti la Serikali Na. 57 na marekebisho ya Kanuni tajwa kupitia Gazeti la Serikali Na. 761A la tarehe 30 Oktoba 2023 na Mabadiliko ya Kanuni za Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja za Mwaka 2024. - d) Vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana yakionesha bei za mafuta, punguzo, vivutio
vya kibiashara vinavyotolewa na kituo husika. Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta katika vituo vinavyouza mafuta kwa bei nafuu zaidi ili kushamirisha ushindani. Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja. Adhabu kali itatolewa kwa kituo husika kwa kutotekeleza matakwa
ya kisheria kwa mujibu wa kanuni husika. - e) Wauzaji wa bidhaa za mafuta ya petroli wanatakiwa kutoa stakabadhi za mauzo
kutoka kwenye Electronic Fiscal Pump Printers (EFPP) na wanunuzi
wahakikishe wanapata stakabadhi hizo za malipo zinazoonyesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita. Stakabadhi hizo zitatumika kama kidhibiti kwa wanunuzi wa mafuta endapo kutajitokeza malalamiko ya kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko bei kikomo au kuuziwa
mafuta yasiyo na kiwango cha ubora unaotakiwa. Stakabadhi hizo pia zitasaidia kurahisisha ukusanyaji wa kodi za Serikali zitokanazo na mauzo ya
bidhaa za mafuta ya petroli.
BEI MPYA ZA MAFUTA KUANZIA LEO JUMATANO JULY 03-2024 DOWNLOAD PDF HAPA.
BEI ZA MAFUTA YA PETROLI KWA MWAKA 2024
Cap Prices for Petroleum Products wef 3rd July 2024-Kiswahili
Cap Prices for Petroleum Products wef 3rd July 2024- English
Cap Prices for Petroleum Products wef 5th June 2024 -Kiswahili
Cap Prices for Petroleum Products wef 5th June 2024 – English
Cap Prices for Petroleum Products wef 1st May 2024 -Kiswahili
Cap Prices for Petroleum Products wef 1 st May 2024 – English
Cap Prices for Petroleum Products wef 3rd April 2024 -Kiswahili
Cap Prices for Petroleum Products wef 3rd April 2024 – English
Cap Prices for Petroleum Products wef 6th March 2024 – Kiswahili
Cap Prices for Petroleum Products wef 6th March 2024 – English
Cap Prices for Petroleum Products wef 7th February 2024 – Kiswahili
Cap Prices for Petroleum Products wef 7th February 2024 – Kiswahili
Cap Prices for Petroleum Products wef 3rd January 2024 – Kiswahili
Cap Prices for Petroleum Products wef 3rd January 2024- English
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), ni taasisi ya udhibiti wa huduma za nishati na maji inayojitegemea, iliyoundwa kwa Sheria ya EWURA Sura ya 414 ya Sheria za Tanzania na marekebisho yake Na. 6 ya mwaka 2019.
EWURA, ilianza kazi rasmi Septemba, 2006 ikiwa na wajibu wa kusimamia shughuli zote za kiuchumi na kiufundi katika sekta za Nishati(umeme, petroli na gesi asilia); na Maji (majisafi na usafi wa mazingira).
Katika kutekeleza wajibu wake, kwa uwazi na kwa manufaa ya wote, EWURA inazingatia sheria za kisekta, sera na miongozo ifuatayo:-
Sera ya Taifa ya Nishati (2015), Sera ya Taifa ya Maji (2002), Sheria ya EWURA, Sura Na. 414; Sheria ya Umeme, Sura Na. 131; Sheria ya Petroli, Sura Na. 392; Sheria ya Maji na Usafi wa Mazingira, Sura Na. 279; kanuni na miongozo mbalimbali.
Dira ya EWURA
Kuwa Mdhibiti wa Kiwango cha Kimataifa kwa Huduma Endelevu za Nishati na Maji
Dhamira ya EWURA
Kudhibiti huduma za nishati na maji kwa uwazi, ufanisi na tija ili kuhakikisha ubora, upatikanaji na unafuu wa huduma hizo
Kazi na Majukumu ya EWURA
Kwa mujibu wa Kifungu cha 7 cha Sheria ya EWURA, majukumu ya Mamlaka niajukumu hayo ni:-
- Kutekeleza kazi zote zilizoanishwa kwenye sheria ya EWURA na Sheria za Kisekta;
- Kutoa, kuhuisha na kufuta leseni;
- Kuweka na kusimamia viwango vya ubora wa huduma;
- Kudurusu na kusimamia bei za huduma,
- Kutunga sheria ndogo na kanuni;
- Kufuatilia maendeleo ya sekta zinazodhibitiwa kwa kuzingatia upatikanaji, ubora wa huduma, gharama ya huduma, ufanisi wa uzalishaji, uwekezaji na usambazaji wa huduma;
- Kusimamia utatuzi wa malalamiko na migogoro;
- Kutoa taarifa kuhusu kazi za udhibiti;
- Kupata maoni ya mamlaka zingine za kiudhibiti; na
- Kusimamia utekelezaji wa Sura Na 414 ilyoianzisha EWURA.
Katika kutekeleza kazi zake, EWURA ina wajibu wa kukuza ustawi wa Watanzania kwa kuzingatia yafuatayo:-
- Kuhimiza ushindani wenye tija na ufanisi kiuchumi;
- Kulinda maslahi ya walaji;
- Kulinda mitaji ya kifedha ya watoa huduma;
- Kuhimiza upatikanaji wa huduma zinazodhibitiwa kwa makundi yote ikiwamo wenye vipato vya chini,makundi maalumu na vijijini;
- Kuimarisha utoaji wa elimu kwa umma na kujenga uelewa kuhusu sekta zinazodhibitiwa, ikiwamo haki na wajibu wa watumiaji na watoa huduma zinazodhibitiwa, namna ya kupokea na kutatua malalamiko na migogoro na kazi, wajibu na shughuli za Mamlaka;
- Kulinda na kutunza mazingira.
Soma Zaidi:-https://www.ewura.go.tz/fuel-prices/
Bei ya mafuta ya diesel leo July 2024, Bei ya mafuta ya petrol July 2024, Ewura bei mpya July 2024,bei ya petrol Dar es Salaam July 2024,Bei ya mafuta leo tanzania Julai 2024,Bei Kikomo za Bidhaa za Mafuta ya Petroli kuanzia Jumatano tarehe 03-2024 saa 6:01 usiku, Jinsi ya kuangalia bei za mafuta Tanzania, Bei ya mafuta leo tanzania, Bei za mafuta July 2024.
Tags: Bei Kikomo za Bidhaa za Mafuta ya Petroli kuanzia Jumatano tarehe 03-07-2024., Energy and Water Utilities Regulatory Authority, EWURA Bei Mpya ya Mafuta Kuanzia July 03-2024, EWURA Bei Mpya za Mafuta Tanzania July 03-2024, EWURA New Fuel Price Tanzania July 2024, New Fuel Price Tanzania July 5-2024