JEAN Charles Ahoua ni Mnyama
JEAN Charles Ahoua ni Mnyama
JEAN Charles Ahoua ni Mnyama,Klabu ya Simba imekamilisha usajili Kiungo Mshambuliaji, Ahoua Jean Charles raia wa Ivory Coast kwa mkataba wa miaka miwili.
Ahoua mwenye umri wa miaka 22 ametua Simba akitokea klabu ya Stella Club d’Adjamé ya nchini kwao Ivory Coast.JEAN Charles Ahoua ni Mnyama.
Ohoua ndiye anayetazamwa kuwa mrithi sahihi wa Clatous Chama baada ya msimu uliopita kuibuka mchezaji bora (MVP), wa Ligi Kuu ya Ivory Coast alikofunga mabao 12 na kutoa pasi za mabao tisa.
Ahoua anasifika kwa kufunga mabao kutoka umbali mrefu, kuchezesha timu pamoja kutengeneza nafasi kwa wenzie.
Kuelekea msimu wa Ligi 2024/25 Simba imekuja utaratibu mpya kwenye usajili wa kuingiza wachezaji bora wenye uwezo na umri mdogo ili kujenga timu imara ya muda mrefu.
Ahoua anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa na Simba baada ya beki wa kati, Lameck Lawi Kutoka Coastal Union, winga Joshua Mutale kutoka Power Dynamos na Mshambuliaji Mganda Steven Dese Mukwala kutoka Asante Kotoko ya Ghana.
Upande wa Wachezaji waliopewa Thank You hadi sasa ni aliyekuwa nahodha wa timu hiyo John Bocco, Saido Ntibazonkiza, Shaaban Idd Chilunda, Luis Miquissone, Kennedy Juma na Henock Inonga aliyeuzwa FAR Rabat ya Morocco huku Clatous Chama akijiunga na Young Africans.
Tags: AHOUA Jean Charles ni Mnyama, JEAN Charles Ahoua ni Mnyama