RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI za Madereva Kutoka Wilaya ya Shinyanga July 04-2024

Filed in Ajira by on 05/07/2024

NAFASI za Madereva Kutoka Wilaya ya Shinyanga July 04-2024

NAFASI za Madereva Kutoka Wilaya ya Shinyanga July 04-2024, Ajira za Madereva Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Leo July 04-2024, Nafasi za Kazi za Madereva Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Leo tarehe 04-07-2024.

NAFASI za Madereva Kutoka Wilaya ya Shinyanga July 04-2024

NAFASI za Madereva Kutoka Wilaya ya Shinyanga July 04-2024, Ajira za Madereva Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Leo July 04-2024, Nafasi za Kazi za Madereva Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Leo tarehe 04-07-2024.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga amepokea Kibali cha Ajira Mpya kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kupitia Barua yenye Kumb.Na.FA.97/228/01/09 ya tarehe 25.06.2024.

Hivyo, anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi zifuatazo:

✅DEREVA DARAJA LA II (NAFASI 03)

SIFA ZA KUAJIRIWA.
Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Sita (Form Six), Awe na leseni ya
Daraja la C au E ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali.

Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Cource) yanayotolewa na chuo cha VETA au NIT au Chuo kingine kinachotambulika na Serikali.

KAZI NA MAJUKUMU YA DEREVA DARAJA LA II

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;
  • Kupeleka watumishi kwenye safari za kazi;
  • Kufanya matengenezo madogomadogo ya gari;
  • Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali;
  • Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari; na
  • Kufanya usafi wa gari.

MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B

MASHARTI YA JUMLA

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini;
  • Waombaji wawasilishe maelezo binafsi (Curriculum Vitae) yanayojitosheleza (Detailed CV) yenye Anuani na Namba za simu za kuaminika pamoja na majina
    ya wadhamini watatu (Referees) wa kuaminika.
  • Waombaji waambatanishe nakala za vyeti vya Kidato cha Nne au Sita, Taaluma na cheti cha kuzaliwa. Waombaji watakaowasilisha” Result Slip”,” Statement of
    Results”,” Provisional Results” au” Transcripts HAVITAKUBALIKA.
  • Kwa Waombaji waliosoma nje ya Nchi, Elimu ya Kidato cha Nne au Sita wawasilishe uthibitisho kutoka Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA).
  • Kwa waombaji waliosoma Vyuo nje ya Nchi wawasilishe uthibitisho kutoka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).
  • Waombaji watakokidhi sifa zinazotakiwa ndio watakaoitwa katika usaili.
  • Barua ya maombi iliyosainiwa na Mwombaji inaweza kuandikwa kwa lugha ya Kiingereza au Kiswahili.
  • Waombaji wenye mahitaji maalum (special needs/disability) wanatakiwa kuainisha kwenye maombi yao.
  • Waombaji watakaowasilisha Taarifa za kughushi watachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria za Nchi.
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.

Mwisho wa kuwasilisha maombi ni tarehe 18 Julai, 2024.Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment
Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).

Maombi yatakayowasiIishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

Tags: , ,

Comments are closed.