NAFASI za Madereva Kutoka Wilaya ya Kishapu July 04-2024
NAFASI za Madereva Kutoka Wilaya ya Kishapu July 04-2024
NAFASI za Madereva Kutoka Wilaya ya Kishapu July 04-2024, Nafasi za Madereva Kutoka Halmashauri Wilaya ya Kishapu Leo July 04-2024, Ajira za Madereva Kutoka Halmashauri Wilaya ya Kishapu July 04-2024.
Kwa mujibu wa kibali cha ajira mbadala chenye Kumb. Na. FA.97/288/01/09 cha tarehe 25 Juni, 2024 kutoka Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu anawatangazia wananchi wote Raia wa Tanzania kuomba nafasi za Kazi zifuatazo:-
✅DEREVA DARAJA LA II (NAFASI 3)
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Sita (Form Six), Awe na leseni ya
Daraja la C au E ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda
usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Cource) yanayotolewa na chuo cha VETA au NIT au Chuo kingine kinachotambulika na Serikali.
KAZI NA MAJUKUMU YA DEREVA II
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;
- Kupeleka watumishi kwenye safari za kazi;
- Kufanya matengenezo madogomadogo ya gari;
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali;
- Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari; na
- Kufanya usafi wa gari.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B
MASHARTI YA JUMLA
- Mwombaji awe Raia wa Tanzania ambaye ana umri si zaidi ya Miaka 45 na sio pungufu ya Miaka 18.
- Mwombaji aambatishe nakala ya Cheti cha kuzaliwa.
- Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya Wadhamini (referees) watatu wa kuaminika pamoja na namba zao za Simu.
- Maombi yote yaambatane na nakala za vyeti vya Elimu na taaluma kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, na vilivyothibitishwa na Wakili au
Kamishna wa Viapo. - Testimonials, provision results, statement of results, havitakubaliwa
- Waombaji wote ambao wamesoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao
vinafanyiwa ulinganishi na TCU na NACTE. - Waomabji waambatanishe picha moja passport size ya hivi karibuni
- Barua ya Maombi iandikwe kwa Kiswahili au Kingereza
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 17 Julai, 2024.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamoja na vyeti, aidha anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya,
S.L.P 1288,
KISHAPU.
Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye Mfumo wa Kieletroniki wa Ajira
(Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo: https://portal.ajira.go.tz/ anuani
hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Secretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu
iliyoandikwa “Recruitment Portal”
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioanishwa katika tangazo hili
HAYATAFIKIRIWA.
POST: DEREVA DARAJA II – 3 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu More Details |
2024-07-17 Login to Apply |
Tags: Ajira za Madereva Kutoka Halmashauri Wilaya ya Kishapu July 04-2024., Nafasi za Madereva Kutoka Halmashauri Wilaya ya Kishapu Leo July 04-2024, NAFASI za Madereva Kutoka Wilaya ya Kishapu July 04-2024