NEC Walioitwa Kwenye Usaili Jimbo la Nsimbo July 2024
NEC Walioitwa Kwenye Usaili Jimbo la Nsimbo July 2024
NEC Walioitwa Kwenye Usaili Jimbo la Nsimbo July 2024, Majina ya Walioitwa kwenye Usaili NEC Jimbo la Nsimbo Mkoa wa Katavi July 07-2024, Majina Mapya ya Walioitwa kwenye Usaili NEC Jimbo la Nsimbo Katavi , Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili NEC Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo July 07-2024.
TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI ZA WAANDISHI WASAIDIZI NA WAENDESHA VIFAA VYA BVR KIT
Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Uchaguzi Nsimbo Mkoa wa Katavi anawatangazia waombaji kazi nafasi za Mwandikishaji Msaidizi na Mwendesha BVR Kufika kwenye usaili utaokaofanyika tarehe 11/07/2024.
Wasailiwa walioitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
- Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwaajili ya utambuzi,
- Vitambulisho mfano kitambulisho cha mkaazi, kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha Uraia, Hati ya Kusafiria au kitambulisho cha kazi.
- Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI (original), kuanzia cheti cha kuzaliwa,na vile ambavyo uliambatanisha kwenye barua ya maombi.
- Aidha kila msailiwa atajigharamia chakula, usafiri na malazi.
- Kila msailiwa azingatie tarehe na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
Vituo vya usaili na maelezo mengine yanapatikiana kwenye viunganishi vya kata hapa chini
- KUITWA KWENYE USAILI KATA YA IBINDI.pdf
- KUITWA KWENYE USAILI KATA YA ITENKA.pdf
- KUITWA KWENYE USAILI KATA YA KANOGE.pdf
- KUITWA KWENYE USAILI KATA YA KAPALALA.pdf
- KUITWA KWENYE USAILI KATA YA KATUMBA.pdf
- KUITWA KWENYE USAILI KATA YA LITAPUNGA.pdf
- KUITWA KWENYE USAILI KATA YA MACHIMBONI.pdf
- KUITWA KWENYE USAILI KATA YA MTAPENDA.pdf
- KUITWA KWENYE USAILI KATA YA NSIMBO.pdf
- KUITWA KWENYE USAILI KATA YA SITALIKE.pdf
- KUITWA KWENYE USAILI KATA YA URUWIRA.pdf
- KUITWA KWENYE USAILI KATA YA UGALLA.pdf
NEC Walioitwa Kwenye Usaili Jimbo la Nsimbo July 2024
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imesema watu wote wenye sifa za kuandikishwa kuwa wapiga kura wataandikishwa hata kama hawana kitambulisho cha Taifa kinachotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bi. Giveness Aswile tarehe 15 Juni, 2024 jijini Dar es Salaam wakati akiwasilisha mada kwenye mkutano wa Tume na Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri.
Mkutano huo unahitimisha mfululizo wa mikutano ambayo Tume imefanya na wadau wake kauanzia tarehe 07 Juni, 2024. Baadae Tume itafanya mikutano na wadau kwenye mikoa yote kwa kuzingatia ratiba ya uboreshaji wa Daftari.
Mikutano hiyo ina lengo Ia kuwapa wadau taarifa za uwepo wa zoezi la uboreshaji wa Daftari Ia Kudumu la Wapiga Kura na kuwapitisha katika vifaa na mifumo ya uandikishaji pamoja na kuona namna zoezi litakavyofanyika vituoni.
“Kuwa na kadi ya NIDA sio kigezo cha kuandikishwa kwenye Daftari la Kudumu Ia Wapiga Kura. Wananchi wote wenye sifa wataandikishwa bila kujali kama wana kadi ya NIDA au la,” amesema Bi. Aswile.
Ameyataja mambo yatakayohusika kwenye uboreshaji wa daftari kuwa ni pamoja na kuandikisha wapiga kura wapya ambao ni raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na zaidi na watakaotimiza umri huo ifikapo tarehe ya uchaguzi mkuu 2025 na kutoa fursa kwa wapiga kura waliopo kwenye daftari na ambao wamehama, waweze kuhamisha taarifa zao kutoka kata au jimbo walioandikishwa awali.
Mambo mengine ni kutoa fursa kwa wapiga kura walioandikishwa kurekebisha taarifa zao yakiwemo majina na taarifa nyingine, kutoa kadi mpya kwa wapiga kura waliopoteza kadi au kadi zao kuharibika na kuondoa wapiga kura waliopoteza sifa za kuwemo kwenye Daftari kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuukana uraia wa Tanzania au kifo.
Tags: Majina Mapya ya Walioitwa kwenye Usaili NEC Jimbo la Nsimbo Katavi, Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili NEC Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo July 07-2024., Majina ya Walioitwa kwenye Usaili NEC Jimbo la Nsimbo Mkoa wa Katavi July 07-2024, NEC Walioitwa Kwenye Usaili Jimbo la Nsimbo July 2024