RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


WANAFUNZI zaidi ya laki moja Wafaulu Matokeo ya Form Six 2024

Filed in Habari by on 13/07/2024

WANAFUNZI zaidi ya laki moja Wafaulu Matokeo ya Form Six 2024

WANAFUNZI zaidi ya laki moja Wafaulu Matokeo ya Form Six 2024

WANAFUNZI zaidi ya laki moja Wafaulu Matokeo ya Form Six 2024

WANAFUNZI zaidi ya laki moja Wafaulu Matokeo ya Form Six 2024,Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) Limetangaza Matokeo ya mtihani wa kidato cha Sita uliofanyika May mwaka huu 2024 ambapo jumla ya Watahiniwa 111,056 wa Shule na kujitegemea sawa na 99.43% ya Watahiniwa wenye matokeo ya mtihani huo wamefaulu.

Akitangaza matokeo hayo leo Jumamosi July 13,2024 Katika Ofisi za NECTA Visiwani Zanzibar, Katibu Mtendaji wa NECTA, Dr. Said Mohamed, amesema kuwa “Wanawake waliofaulu ni 49,837 sawa na 99.61% wakati Wanaume waliofaulu ni 61,219 sawa na 99.28%, mwaka 2023 Watahiniwa waliofaulu walikuwa ni 104,549 sawa na 99.23%, hivyo ufaulu wa jumla umeongezeka kwa 0.20% ikilinganishwa na mwaka 2023”

“Watahiniwa wa Shule waliofaulu ni 103,252 sawa na 99.92% ya Watahiniwa wenye matokeo, Wanawake waliofaulu ni 46,615 sawa na 99.93% na Wanaume ni 56,637 sawa na 99.91%, Watahiniwa walioshindwa mtihani ni 84 sawa na 0.08%, mwaka 2023 watahiniwa 96,010 sawa na asilimia 99.90 ya Watahiniwa wa Shule walifaulu mtihani huo, hivyo ufaulu wa Watahiniwa wa Shule umeongezeka kwa 0.02% ikilinganishwa na mwaka 2023”

“Idadi ya Watahiniwa wa kujitegemea waliofaulu mtihani ni 7,804 sawa na 93.34%, mwaka 2023 Watahiniwa wa kujitegemea 8,539 sawa na 92.30% walifaulu mtihani huo, hivyo ufaulu wa Watahiniwa wa kujitegemea umeongezeka kwa 1.04% ikilinganishwa na mwaka 2023”

Tags:

Comments are closed.