NAFASI 10 za Kazi Wilaya ya Mbarali July 15-2024
NAFASI 10 za Kazi Wilaya ya Mbarali July 15-2024
NAFASI 10 za Kazi Wilaya ya Mbarali July 15-2024,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali amepokea kibali cha Ajira mpya kwa ikama ya mwaka 2023/2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye Kumb.Na.FA.97/288/01/09 cha tarehe 25/06/2024.
Hivyo Watanzania wote wenye sifa wanatangaziwa kutuma maombi ya kazi kwa nafasi zifuatazo:-
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI 15-07-2024
✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – NAFASI 05
MAJUKUMU YA KAZI
- Kuorodhesha barua zinazoingia masijala kwenye Regista (Incomming);
- Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya Taasisi (Outgoing Correspondence Register);
- Kusambaza majalada kwa watendaji (ActionOfficers);
- Kupokea majalada yanayorudi masijala kutoka kwa watendaji;
- Kutafuta kumbukumbu / Nyaraka au majalada yanayohitajika na watendaji;
- Kurudisha majalada kwenye shubaka/kabati la majalada
(Racks/Filling Cabinets) au Mahali Pengine yanapohifadhiwa; na
Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani na nje ya Taasisi (File tracking).
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI) aliyehitimu
Stashahada (NTA level 6) katika fani ya Masjala kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, mwenye ujuzi wa Kompyuta.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali –TGSC
✅DEREVA DARAJALA II – NAFASI 05
MAJUKUMU YA KAZI
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari
- Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari
za kikazi; - Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari;
- Kutunza na kuandika daftari la safari “logbook” kwa safari zote.
- Kufanya usaf iwa Gari; na
- Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe na cheti cha Mtihani wa Kidato cha Nne (IV),mwenye leseni Daraja ‘C’ au ‘E’ ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua Mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali, Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji Magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) au
NIT au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia viwango vya Serikali – TGS B
MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi waUmma.
- Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (Detail Curriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya Barua Pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
- Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia Sifa za kuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi ya kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo. - Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/ Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
- Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI,-Computer Certificate,-Vyeti vya Kitaaluma (Professional Certificate from Respective Boards);
- Testmonial“, ‘‘Provisional Results“, “Statement of results“, hati ya matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (NECTAna NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishiwa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika
Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010. - Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 28 Julai, 2024.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa: –
MKURUGENZI MTENDAJI,
HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI,
S.L.P 237, RUJEWA
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment
Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).
Maombi yatakayowasiIishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
DONWLOAD PDF DOCUMENT
POST: DEREVA DARAJA II – 5 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali More Details |
2024-07-28 Login to Apply |
POST: MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – 5 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali More Details |
2024-07-28 Login to Apply |