YANGA Kucheza na Augsburg ya Bundesliga
YANGA Kucheza na Augsburg ya Bundesliga
YANGA Kucheza na Augsburg ya Bundesliga,Kikosi cha Yanga kitaanza safari Leo Alhamisi kuelekea Afrika Kusini kwaajili ya kushiriki Michuano Maalum ya Pre-Season ambayo wamealikwa.
Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ali Kamwe amesema kuwa Yanga itashiriki Michuano ya Mpumalanga Premier’s International Cup ambapo itacheza mechi mbili.
Michuano hiyo imedhaminiwa na Shirika la Utangazaji la Afrika Kusini (SABC) kwa Kushirikiana na TS Galaxy Foundation.
Ni michuano Maalum ya Pre-season ambayo pamoja na Yanga, timu nyingine zitakazoshiriki ni TS Galaxy Fc, Mbabane Swallows FC na Augsburg inayoshiriki Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga)
Augsburg ilianzishwa mwaka 1907, ni klabu kubwa zaidi ya Soka katika Swabian Bavaria yenye wanachama 25,000 na ilipanda Ligi Kuu ya Bundesliga kwa mara ya kwanza mwaka 2011, ambako imebaki tangu wakati huo.
Mchezo wa kwanza utakuwa ni Julai 20 dhidi ya Augsburg inayoshiriki Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga), mchezo huo utahudhuriwa na Mashabiki na kuonyeshwa Mbashara na vituo vya Televisheni.
Mchezo wa pili utapigwa Julai 24 dhidi ya Ts Galaxy ya Afrika Kusini. Mchezo huo hautahudhuriwa na Mashabiki wala kurushwa Mbashara na Vituo vya Televisheni.
Aidha Julai 28 Yanga itacheza mchezo wa tatu dhidi ya Kaizer Chiefs katika Michuano ya Toyota Cup 2024.
Baada ya Michezo hiyo mitatu nchini Afrika Kusini, Yanga itarejea Jijini Dar es salaam Julai 30 kwaajili ya maandalizi ya mwisho kuelekea Kilele cha Wiki ya Mwananchi August 04-2024.