MAMBO Muhimu unapoitwa kwenye Usaili UTUMISHI
MAMBO Muhimu unapoitwa kwenye Usaili UTUMISHI
MAMBO Muhimu unapoitwa kwenye Usaili UTUMISHI, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma – Ndicho chombo pekee kwa mujibu wa sheria chenye Mamlaka ya kuajiri watu katika Utumishi wa Umma kwa kuzingatia SERA, SHERIA, KANUNAI, NA TARATIBU zinazohusu Ajira katika Utumishi wa Umma.
Mchakato wa Ajira katika Utumishi wa
Umma unazingatia sifa, taaluma, ushindani, uwazi, na usawa kwa mujibu wa SERA, SHERIA, KANUNI, NA TARATIBU zinazohusu Ajira katika Utumishi wa Umma Sekretarieti ya Ajira huendesha saili mbalimbali ili kupata
wataalamu wenye tija kulingana
na nafasi za ajira zilizotangazwa.
Saili za vitendo hufanyika kwa kada zenye mahitaji ya kubaini uwezo wa kutumia nyenzo mahsusi, ili kupima uwezo wa ujuzi wa utendaji kazi.
Ni muhimu kupakia taarifa binafsi na za
kitaaluma kwenye mfumo wa AJIRA PORTAL ili kuweza kuomba kazi pindi zitakapotangazwa.
Nyaraka Muhimu wakati unaenda kwenye Usaili Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
- Cheti halisi cha kuzaliwa
- Kitambulisho cha Taifa, Kitambulisho Cha Mkazi, Hati ya kusafiria, Kadi ya Mpiga Kura, Leseni ya Udereva au Barua kutoka Serikali ya Mtaa
- Vyeti halisi vya kitaaluma
- Hati ya kiapo, endapo majina yanatofautiana kwenye nyaraka.
Mawasiliano
026 2160350
Tembelea – www.ajira.go.tz Kupata Ajira zote zinazotangazwa Kila Siku Kutoka UTUMISHI.