RC Mwassa Awataka Viongozi wa Dini Kuwaombea Waumini Wajiepushe na Matendo ya Kikatili
RC Mwassa Awataka Viongozi wa Dini Kuwaombea Waumini Wajiepushe na Matendo ya Kikatili
RC Mwassa Awataka Viongozi wa Dini Kuwaombea Waumini Wajiepushe na Matendo ya Kikatili,Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe Hajat Fatma Mwassa amewaomba Viongozi wa madhehebu ya Dini kuendelea kuwalea kimaadili waumini wao jambo ambalo litasaidia kuepukana na Vitendo vya Kikatili.
Bi. Hajat Mwassa ametoa wito huo wakati wa Ibada ya Shukrani ya Uchungaji pamoja na Maombezi Maalum ya Kuliombea Taifa na Viongozi, iliyofanyika katika Viwanja vya Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Lweru Wilayani Muleba mapema Julai 28, 2024 wakati alipoambatana na Mgeni Rasmi Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa kwa niaba ya Waziri Mkuu.
Katika Mkoa wetu wa Kagera kuna mshikamano mkubwa wa viongozi wa Dini zote na leo hii mshikamano huo unaonekana mahala hapa, Baba Askofu Mbelwa kawaalika Viongozi wa Dini nyingine na kuungana naye ili kumwombea Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na wasaidizi wake kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa misingi ya haki, Utawala bora, hekima na busara.
Tunapowaombea Viongozi wetu wa Kitaifa na kuliombea amani na utulivu Taifa letu la Tanzania nitumie fursa hii pia kuwakumbusha ninyi Viongozi wetu wa Dini kuendelea kukemea vikali vitendo vya kikatili katika jamii zetu hususani ukatili kwa watoto. Niwaombe muendelee kuwahubiri waamini wetu katika nyumba zetu mbalimbali za ibada Wananchi kutojihusisha na vitendo hivyo vya ukatili kwa binadamu wenzetu.” Amesema Hajat Mwassa
Ibada hiyo imeambatana na Harambee ya Ujenzi wa Makao Makuu ya Kanisa hilo Mkoani Kagera ambapo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa imechangia shilingi Milioni Moja.
Tags: RC Mwassa Awataka Viongozi wa Dini Kuwaombea Waumini Wajiepushe na Matendo ya Kikatili