RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


VIGEZO vya kuwa Wakala wa CRDB Bank

Filed in Makala by on 29/07/2024

VIGEZO vya kuwa Wakala wa CRDB Bank

VIGEZO vya kuwa Wakala wa CRDB Bank

VIGEZO vya kuwa Wakala wa CRDB Bank

VIGEZO vya kuwa Wakala wa CRDB Bank, CRDB Wakala ni wakala wa Benki ya CRDB chini kitengo cha idara ya wateja wadogo.

CRDB imekua mbele kiubunifu katika utoaji huduma za kifedha nchini kwa kua Benki ya kwanza kuanzisha huduma ya uwakala nchini Tanzania mwaka 2013 iliyokua ikijulikana kama “Fahari Huduma Wakala”.

CRDB Wakala ni wakala wa kibenki waliopitishwa na kufundishwa utoaji huduma za kifedha kwa niaba ya Benki ya CRDB kulingana na kanuni na mwongozo wa Benki kuu ya Tanzania.

Mtandao wa CRDB Wakala unawawezesha watanzania wote walio wateja na wasio wateja wa kibenki kupata huduma zetu za kifedha kiurahisi popote walipo.

Huduma zinazopatikana kwa CRDB Wakala

  • Maulizo ya salio na taarifa fupi za kibenki.
  • Kuweka pesa kwenye akaunti yoyote ya CRDB bila makato yoyote.
  • Kutoa pesa kutoka kwenye akaunti ya CRDB kwa kutumia kadi yoyote ya CRDB au SimBanking ( App au kwa kupiga *150*03#).
  • Malipo ya huduma mbalimbali kama bili ya LUKU, maji, tiketi za kusafiria, ving’amuzi, muda wa maongezi na mengine.
  • Malipo ya Ada za shule.
  • Malipo ya mikopo, ustaafu na huduma za kijamii.
  • Malipo ya Serikali kupitia namba za malipo ya GePG na TRA.
  • Kufungua akaunti mpya ya CRDB papo hapo.
  • Kujisajili kupata TemboCard

Faida ya CRDB Wakala kwa mteja ni kama yafuatayo

  • Okoa Muda : Huduma za mawakala wetu hazina foleni hivyo ni haraka zaidi na kwa uhakika
  • Okoa Gharama : Tumekuondolea hitaji la kwenda umbali mrefu kupata huduma zetu za kifedha, sasa imekua rahisi zaidi mtaani karibu na makazi ya watu.
  • Ongezeko la muda wa huduma za kibenki : Tofauti na matawini ambapo kuna muda malumu wa utoaji huduma, CRDB Wakala inatoa huduma takati wowote.
  • Ujuzi wa huduma za kibenki : CRDB Wakala kama mabalozi wetu wanashiriki katika utoaji maarifa ya huduma zetu na bidhaa kwa wateja.
  • Mawakala wetu kwa njia ya kukubali amana ya pesa wanapunguza hatari kwa wateja wetu wanaotamani kuweka amana kabla ya kusafiri.
  • Mtandao wetu mpana wa CRDB Wakala wenye zaidi ya mawakala 14,000 umetusaidia kufika kila kona ya Tanzania.

VIGEZO vya kuwa Wakala wa CRDB BankBenki ya CRDB pia imekubaliana na Shirika la Posta Tanzania kuwa mmoja wa mawakala wetu kwa kuturuhusu kutumia maduka yao nchini kote kutoa huduma ya CRDB tangu 2013.

Benki ya CRDB kupitia mtandao wa CRDB Wakalas imetoa fursa ya ajira kwa zaidi ya Watanzania 25,000 waliojitolea kutoa huduma za kibenki kwa niaba ya Benki ya CRDB.

CRDB inakaribisha mfanyabiashara yeyote mwenye uwezo ajiunge na jitihada zetu za kutoa huduma za kibenki kwa urahisi kila mahali na kupata faida kubwa zaidi.

Faida Kuboresha Chapa ya Benki ya CRDB kwa kufanya kazi na Taasisi inayoongoza na inayofanyakazi ya Kifedha Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Pata kamisheni ya kuvutia kwa kutoa huduma kwa Wateja Wakubwa nchini kote. Ongeza Wateja katika biashara yako ya awali kwa kuwa wateja wa CRDB watatembelea eneo lako hivyo kuongeza mauzo, Leta ufanisi kwenye biashara yako kwenye usimamizi wa fedha kwani utakuwa unahudumia Wateja wa CRDB wanaotoa fedha hivyo kupunguza hatari ya fedha taslimu.

Jenga Uwezo kupitia Benki za CRDB kuwajengea uwezo Mafunzo ya Bure katika maeneo ya Wajasiriamali, Huduma za Kibenki, Ufuaji na Kupambana na Udanganyifu.

BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD FOMU YA MAOMBI YA KUWA WAKALA WA CARD BANK

Kwa Maelezo zaidi Tembelea Tawi la CRDB Katika eneo lako.

Tags:

Comments are closed.