NACTVET Yafanya Maboresho Mifumo ya Kieletroniki
NACTVET Yafanya Maboresho Mifumo ya Kieletroniki
NACTVET Yafanya Maboresho Mifumo ya Kieletroniki,Taarifa kwa Umma Kuhusu Maboresho ya Mifumo ya Kieletroniki Ya NACTVET.
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) linapenda kuutaarifu umma kuwa kutokana na mabadiliko ya mawasiliano kutoka kwa mtoa huduma za mtandao wa Baraza (Internet Service Provider), kutakuwa na nyakati za kutopatikana kwa baadhi ya huduma za kimtandao kuanzia tarehe 11 hadi 17 Agosti, 2024.
Lengo ni kuhakikisha huduma za kimtandao zinapatikana kwa ufasaha na kwa wakati.
Huduma zitakazoathirika ni pamoja na:
- Mfumo wa Udahili wa Pamoja (Central Admission System);
- Mfumo wa Ulinganifu wa Tuzo (Foreign Awards Evaluation System);
- Mfumo wa Uombaji Hati ya Matokeo (Transcript Request System); na
- Huduma zinazohusiana na malipo mbalimbali.
Baraza linasisitiza wadau kuomba huduma katika mifumo tajwa hapo juu mapema kabla ya tarehe 11 Agosti, 2024.
Baraza linawahakikishia kwamba maboresho hayo yatakamilika ndani ya muda uliopangwa ili kurejesha huduma zote katika hali ya kawaida.
Baraza linaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza.