UFAHAMU Ugonjwa wa MPOX na Jinsi ya Kujikinga
UFAHAMU Ugonjwa wa MPOX na Jinsi ya Kujikinga
UFAHAMU Ugonjwa wa MPOX na Jinsi ya Kujikinga,Fahamu Kuhusu Ugonjwa wa MPOX na Jinsi ya Kujikinga.
Wizara ya Afya imesema kuwa imejipanga kuudhibiti ugonjwa wa homa ya nyani (Mpox) endapo utaingia nchini.
Kauli ya wizara inatokana na taarifa zinazoeleza kuwa ugonjwa huo upo kusini mashariki mwa nchi jirani ya Kenya.
Taarifa za uwepo wa homa ya nyani nchini Kenya zimeripotiwa baada ya vimelea vya ugonjwa huo kugunduliwa kwa mtu aliyekuwa akisafiri kutoka Uganda hadi Rwanda kupitia Kenya.
Maambukizi mengine ya ugonjwa huo yameripotiwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Burundi na Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Katika taarifa yake Wizara ya Afya imesema kuwa mpaka sasa Tanzania ni salama, na hakuna mtu yoyote aliyepatikana na ugonjwa wa Mpox (awali ulijulikana kama homa ya Nyani) na bado ugonjwa huo haujaingia nchini .
Kufutatia taarifa rasmi iliyolewa na wizara hiyo, ambayo pia ina jukumu la kufuatilia na kutoa taarifa za mwenendo wa magonjwa, hususani yale ya mlipuko pamoja na tetesi za magonjwa ndani na nje ya nchi, imetoa wito kwa wananchi kushirikiana na serikali kuhakikisha ugonjwa hauingii nchini.
Wizara pia imewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari zote dhidi ya ugonjwa huo ikiwemo kuepuka kula, kugusa mizoga au wanyama kama vile nyani au swala wa msituni, kugusa majimaji ya mtu mwenye dalili za ugonjwa wa Mpox.
Homa ya nyani ni nini?
Mpox au Monkeypox ni Ugonjwa wa Virusi unaosababishwa na virusi vya Monkeypox, ambavyo ni jamii ya familia ya virusi vya orthopox vinavyojumuisha virusi vinavyosababisha ndui.
Dalili za ugonjwa wa Mpox
- Homa.
- Maumivu ya Kichwa.
- Vidonda vya Koo.
- Maumivu ya Misuli.
- Uchovu wa mwili.
- Maumivu ya mgongo
- Kuvimba motoki ya mwili.
Dalili nyingine ni; Upele, Malengengele au vidonda kwenye mwili hasa mikononi na miguuni, kifuani, usoni, wakati mwingine sehemu za Siri.
Ugonjwa huu unaambukizwa njia zifuatazo;
- Kula au kugusa mizoga au nyama pori au wanyama pori walioambukizwa mfano nyani, tumbili, sokwe au swala wa msituni.
- Kugusana na mtu mwenye dalili za ugonjwa huu.
- Kugusa majimaji ya mwili wa mtu mwenye maambukizi ya ugonjwa wa Mpox.
- Kugusa vitu vilivyotumiwa na mtu mwenye ugonjwa huu mfano; vyombo, magodoro na matandiko pamoja na nguo zake.
- Kujamiiana na mtu mwenye maambukizi ya ugonjwa wa Mpox.
Jinsi ya Kujikinga na Ugonjwa wa Mpox
- Epuka kugusa majimaji ya mwili Wa mtu mwenye maambukizi ya Mpox
- Epuka kusalimiana kwa kukumbatiana, kubusiana au kushikana mikono na mtu mwenye maambukizi ya Mpox
- Epuka kugusana na mtu mwenye dalili za Ugonjwa wa Mpox
- Nawa mikono yako mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni au tumia vitakasa mikono
- Epuka kula au kugusa mizoga au wanyama pori wenye maambukizi ya Ugonjwa wa Mpox
- Epuka kusogeleana karibu na mtu mwenye dalili za Mpox wakati mnaongea
- Epuka kugusa vyombo, matandiko, nguo au godoro la mtu mwenye Ugonjwa wa Mpox
- Vaa barakoa ikiwa unaongea kwa karibu na mtu aliye na dalili za Mpox Unapo kohoa au kupiga chafya ziba mkono kwa kiwiko
- Safisha na takasa sehemu zote na vitu ambavyo vinaguswa mara kwa mara Epuka kujamiiana na mtu mwenye maambukizi ya ugonjwa huo
Wahi katika kituo cha huduma za afya kwa uchunguzi na matibabu unapoona mojawapo ya dalili za Ugonjwa wa Mpox
Fanya Kweli Usibaki Nyuma Mtu ni Afya
Soma hi pia;