SHINDANO la Kubuni Jina na Nembo ya Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii
SHINDANO la Kubuni Jina na Nembo ya Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii
SHINDANO la Kubuni Jina na Nembo ya Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii, Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa kushirikiana na Wadau wa Sekta ya Afya inatekeleza mikakati mbalimbali inayolenga kuimarisha Mifumo ya kutolea huduma za Afya za msingi katika ngazi ya Jamii.
Mojawapo ya mikakati hiyo ni kuimarisha huduma za Afya zinazotolewa na Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii (CHWs) kwa kutekeleza Mpango Jumuishi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii.
Mpango huu unalenga kuongeza tija na ufanisi wa Watoa hudumu za Afya ngazi ya jamii kwa kuboresha Uratibu, Mafunzo na Usimamizi wa huduma jumuishi zitakazotolewa.
Katika kuendelea na utekelezaji wa Mpango huu, Serikali imepanga kuwa na jumla ya Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii 137,294 kutoka katika Mitaa na Vitongoji vyote nchi nzima.
Wahudumu hawa watafanya kazi ya kuelimisha na kuhamasisha jamii kupitia njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutembelea kaya, kutoa rufaa kutoka kwenye jamii kwenda katika vituo vya kutolea huduma na kutoa elimu jumuishi ya Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii katika mikusanyiko.
Mpango huu unaambatana na maboresho ya Jina litakalotumiwa na Wahudumu hawa na Nembo itakayotambulisha Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii.
Ili kufanikisha lengo hili Wizara inawakaribisha wataalamu wabunifu kutunga JINA na NEMBO mahususi itakayoakisi shughuli za Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo:-
- Jina na Nembo ziwe zinazoeleweka kirahisi na vya kipekee, Kifupi cha Jina la Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii,
- Jina na Nembo vizingatie maadili ya kitanzania na kuakisi shughuli za Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii,
- Nembo iwe inayoweza kutumika katika nyenzo za mawasiliano mbalimbali za Wahudumu, mfano Majengo, Magari, Nyenzo za mawasiliano na uhamasishaji kama vipeperushi, mabango,tovuti na mitandao ya kijamii.
- Nembo isiwe na uhusiano na kazi yoyote ambayo imewahi kufanyika
MASHARTI:
Mtu yoyote ambaye ni raia wa Tanzania mwenye akili timamu na awe na umri kuanzia miaka 18 anaweza kushiriki katika shindano hili.
Mshiriki atatakiwa kutuma na kutoa maelezo kwa ufupi, mapendekezo ya jina la Wahudumu kwa lugha la Kiswahili pamoja na kifupi chake sambamba na Nembo yenye kuakisi jina hilo.
ZAWADI:
Zawadi nono zitatolewa kwa washindi watatu (3) ambao nembo zao zitaakisi Wahudumu hawa na kazi wanzofanya katika jamii..
Mshindi wa kwanza atazawadiwa fedha taslimu kiasi cha TSH 1,500,000, Mshindi wa pili atazawadia shilingi TSH 1,000,000 na Mshindi wa tatu atazawadiwa shilingi TSH 500,000.
HAKIMILIKI:
Hakimiliki zote za ubunifu wa NEMBO na MAJINA ya Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii zitakuwa ni mali ya washikiri kabla na wakati wa mashindano.
Mara baada ya washindi kupatikana, hakimiliki NEMBO na MAJINA yaliyochaguliwa na washindi kupewa tuzo zitakuwa chini ya Serikali kupitia wizara ya Afya chini ya Idara ya Kinga Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma.
NJIA ZA KUWASILISHA:
Kazi zitumwe kwa njia ya barua pepe [email protected] au [email protected] pamoja Jina la mshiriki na njia za mawasiliano.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na Mratibu wa zoezi hili kwa simu nambari 0716474435.
Mwisho wa kutuma kazi ni tarehe 15 Agosti, 2024.
Tags: SHINDANO la Kubuni Jina na Nembo ya Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii