MAJINA ya Walioitwa kwenye Usaili Ajira za Afya 28 August 2024
MAJINA ya Walioitwa kwenye Usaili Ajira za Afya 28 August 2024,
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya MDAs & LGAs anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 02-09-2024 hadi 12- 09-2024 hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.
Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
- Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.
- Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask)
- Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
- Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura,Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia, Hati ya kusafiria au barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji unachotoka.
- Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa,kidato cha IV, VI, to S Astashahada, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji.
- Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa,kidato cha IV, VI, Astashahada, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji.
- Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hatiza matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI
- Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
- Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
- Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA)
- Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo.
- Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.
- Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.
- Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa iku ya usaili.
- Wasailiwa wote mnajulishwa kuwa hali ya hewa ya Jiji la Dodoma ni baridi hivyo mnashauriwa kuvaa nguo zinazohimili hali ya hewa ya ubaridi.
JINSI ya Kuona Majina ya Walioitwa kwenye Usaili Ajira za Afya 2024 fuata maelekezo haya hapa chini!
- Ingia kwenye mfumo wa UTUMISHI kupitia www.portal.ajira.go.tz
- Login kwenye akaunti yako Kwa kuweka Email/Username na Password
- Nenda sehemu iliyoandikwa My Application
- Kisha utaona ujumbe wa Kuitwa Kwenye Usaili/interview.
- Kama usaili wako una mchujo kwa maana ya Written utafanya usaili kulingana na Current Residential Address yako uliyoijaza wakati wa unaomba Ajira.
- Wale ambao akaunti zao ni ORAL tangazo linasema kuwa ORAL huwa unapangiwa kituo cha usaili Ulipoomba Kazi.
- Mfano wewe ni daktari ila uliomba nafasi ya daktari ukiwa Dar Es Salaam lakini uliomba kwenda kufanya kazi Mkoa wa Mara hivyo Usaili wako wa ORAL utakuwa Mkoani Mara
Pia unasisitizwa kusoma tangazo vizuri.
Siku ya usaili Ajira za afya itakuwa tahere 02/09/2024 (Usaili wa kuandika) na Usaili wa mahojiano utafanyika tarehe 12/09/2024.
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD PDF YA MAJINA KUITWA KWENYE USAILI AJIRA ZA AFYA 28 AUGUST 2024
Tags: MAJINA ya Walioitwa kwenye Usaili Ajira za Afya 28 August 2024