NAFASI za Kazi Mkuranga District Council
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga anawatangazia Watanzania wenye Sifa Kuomba Nafasi za Kazi ya Mkataba ya Kuzika Maiti Wasiotambuliwa (Unclaimed Dead Bodies) Kwa Vigezo Vilivyoainishwa Hapa Chini:
✅Kuzika Maiti Wasiotambulika – Nafasi Mbili (2)
SIFA ZA MWOMBAJI
- Awe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 45.
- Awe amesajiliwa na Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) mwenye kadi au namba ya usajili.
- Awe Mtanzania.
MAJUKUMU YA MZIKA MAITI WASIOTAMBULIKA
- Kuandaa/ kuchimba kaburi kwaajili ya kuzikia
- Kufanya usafi eneo la Hospital Kwa kipindi ambacho haina maiti za kuzika. 3) Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake
JINSI YA KUTUMA MAOMBI:
Barua za maombi zikiwa zimeambatanishwa na Nakala ya kitambulisho cha Nida. picha mbili “Passport size” na namba za simu zitumwe kwa; anuani ya Mkurugezi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga.
Mkurugenzi Mtendaji (W),
Halmashauri ya Wilaya,
S.L.P 10,
Mwisho wa Kupokea Maombi ni tarehe 06/09/2024 SAA 9:30 Alasiri.