KIBU Denis asaini Miwili Simba SC
KIBU Denis asaini Miwili Simba SC
KIBU Denis asaini Miwili Simba SC, hatimaye Klabu ya Simba imefanikiwa kumshawishi Kiungo wake Mshambuliaji, Kibu Denis na kumsainisha Mkataba mpya wa miaka miwili.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya uongozi wa Simba zimethibitisha kuwa Kibu Denis amesaini mkataba wa miaka miwili ambao utamuweka Msimbazi hadi mwaka 2026.
Baada ya majadiliano, uongozi wa Simba umefanya Maboresho makubwa ya Mshahara wake na Fedha za Usajili ambapo imeelezwa nyota huyo ataondoka na kitita cha zaidi ya Tsh Milioni 300 katika miaka miwili.
Aidha klabu za Azam Fc na Yanga zilikaribia kumn’goa Kibu Denis pale Msimbazi kabla ya Simba kuboresha maslahi yaliyomshawishi kuendele kubaki Msimbazi.
Baada ya Kibu Denis, Simba inaendelea na Mazungumzo ya kumuongezea mkataba kiungo wake, Clatous Chama ambapo imeelezwa mazungumzo hayo yako katika hatua za mwisho.
Mwamba huyo wa Lusaka yuko nje ya Uwanja kutokana na majeruhi na anatarajiwa kurejea kikosini pale atakapopona kwani amemaliza adhabu ya kufungiwa mechi tatu.