BAKARI Mwamnyeto Asaini Mkataba Mpya Yanga
BAKARI Mwamnyeto Asaini Mkataba Mpya Yanga
BAKARI Mwamnyeto Asaini Mkataba Mpya Yanga, Nahodha wa Klabu ya Yanga, Bakari Nondo Mwamnyeto ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuwatumikia Wananchi hadi 2026.
Mwamnyeto ni miongoni mwa Wachezaji wa Young Africans ambao mikataba yao ilikuwa imemalizika mwishoni mwa msimu uliomalizika.
Mwamnyeto ambaye ni beki wa kati, safari yake ndani ya kikosi cha Young Africans SC ilianza Agosti 2020 aliposajiliwa akitokea Coastal Union.
Katika misimu minne aliyocheza ndani ya Young Africans SC, Mwamnyeto amechangia kupatikana mataji matatu ya Ligi Kuu Tanzania Bara (2021-2022, 2022-2023 na 2023-2024), mataji matatu ya FA (2021-2022, 2022-2023 na 2023-2024) na Ngao ya Jamii mara mbili (2021-2022 na 2022-2023).
Baada ya mazungumzo na uongozi hatimaye Nahodha huyo wa zamani wa Coastal Union FC ya Tanga ameongeza mkataba huo wa miaka miwili.
Pia amekuwa sehemu ya historia ya Young Africans SC kucheza Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika 2022-2023 ikiwa ni kwa mara ya kwanza ambapo katika michuano hiyo, asisti zake mbili za hatua ya Robo Fainali dhidi ya Rivers United Yanga ikiwa ugenini, zilichangia ushindi wa magoli 2-0 na kufuzu nusu fainali.
Sambamba na msimu uliopita 2023-2024 kucheza Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.