HESLB Nyaraka Zinazohitajika Kwenye Maombi ya Mikopo 2024/2025
HESLB Nyaraka Zinazohitajika Kwenye Maombi ya Mikopo 2024/2025
HESLB Nyaraka Zinazohitajika Kwenye Maombi ya Mikopo 2024/2025, Dirisha la mkopo 2024 2025,Heslb nyaraka zinazohitajika kwenye maombi ya mikopo 2024-2025, Nyaraka za Kuambatanisha kwenye Maombi ya Mikopo HESLB 2024/2025.
Zifuatazo ni nyaraka muhimu za kuambatanisha kwenye maombi ya mkopo:-
- Cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na mamlaka husika, ZCSRA kwa waombaji waliozaliwa Zanzibar au Namba ya Uthibitisho (verification number)
kutoka RITA kwa waombaji waliozaliwa Tanzania Bara; - Vyeti vya vifo kuthibitisha uyatima kutoka mamlaka husika, ZCSRA kwa mzazi/wazazi wa mnufaika waliofariki Zanzibar au Namba ya Uthibitisho kutoka RITA kwa mzazi/wazazi waliofariki Tanzania Bara
- Fomu ya kuthibitisha Ulemavu wa mwombaji (SDF-1) iliyoidhinishwa nabMganga Mkuu wa Wilaya (DMO) au Mganga Mkuu wa Mkoa (RMO);
- Fomu ya kuthibitisha Ulemavu wa mzazi wa mwombaji (PDF-2)
iliyoidhinishwa na Mganga Mkuu wa Wilaya (DMO) au Mganga Mkuu wa Mkoa (RMO); - Fomu ya udhamini (SCSF-3) ikiambatana na uthibitisho wa usaidizi wa kifedha uliopokelewa na mwombaji katika ngazi ya elimu kabla ya chuo. Fomu ya SCSF-3 iidhinishwe na Taasisi mdhamini wa mwombaji;
- Namba ya mnufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF);
- Fomu maalumu ya kituo cha kulelea watoto yatima (SOCF) kuanzia utotoni hadi hatua ya kudahiliwa katika chuo cha elimu ya juu.
- Barua kutoka RITA au ZCSRA ili kuthibitisha taarifa za kuzaliwa kwa waombaji waliozaliwa nje ya nchi. Waombaji ambao mzazi/wazazi wao walifariki nje ya nchi wanapaswa pia kupata barua kutoka RITA au ZCSRA ili kuthibitisha taarifa iliyotolewa;
Soma zaidi; HESLB Muongozo wa Maombi ya Mikopo 2024/2025
Tags: dirisha la mkopo 2024/2025, HESLB Nyaraka Zinazohitajika Kwenye Maombi ya Mikopo 2024/2025, Nyaraka za Kuambatanisha kwenye Maombi ya Mikopo HESLB 2024/2025.