KAMATI ya Uwezeshaji Kibiashara Yatinga Mkoani Kagera
KAMATI ya Uwezeshaji Kibiashara Yatinga Mkoani Kagera
Na Mariam Kagenda _Kagera
KAMATI ya Uwezeshaji Kibiashara Yatinga Mkoani Kagera, Kamati ya Kitaifa ya uwezeshaji wa Kibiashara imefika Mkoani Kagera ili kutembelea vituo vya pamoja vya Forodha vilivyopo Mkoani humo jambo ambalo litasaidia kubaini changamoto mbalimbali zilizopo katika vituo na namna vinavyofanya kazi.
Naibu katibu mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Barozi Dkt John Simbachawene amesema hayo baada ya kamati hiyo kuwasili Mkoani Kagera na kufanya kikao kifupi katika ukumbi wa Mkoa.
Barozi Dkt Simbachawene amesema kuwa kamati hiyo imefika katika Mkoa huo ili kubaini Changamoto zilizoko katika vituo hivyo ili waweze kuzichukua na Serikali iweze kuzifanyia kazi lakini pia nafasi hiyo inawawezesha wajumbe wa kamati hiyo kuona ni kwa namna gani vituo hivyo vinafanya kazi na kuweza kuboresha biashara ikiwa ni pamoja na kuongeza mapato.
Ameongeza kuwa ziara hiyo inaanza leo Julai 16,2024 kwa kuanza kutembelea Bandari Mkoani humo na kuzungumza na wafanyabiashara wa Mkoa huo ambapo watahitimisha ziara Julai 19.
Kwa upande wake Kamishina wa Forodha kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania, Juma Hassan amesema kuwa Tanzania ni sehemu ya nchi ambazo zinasimamia urahisishaji wa Biashara ili wafanyabiashara waweze kufanya biashara zao kwa ufanisi na kutimiza majukumu yao ya kulipa kodi na matakwa mengine ya kisheria yaliyoko ndani ya Biashara.
Kwa upande wake mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Kagera ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Erasto Siima amesema kuwa Mkoa huo unaendelea kufanya kazi vizuri ikiwa ni pamoja na kumsaidia Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan majukumu yanayotakiwa kutekelezwa katika mkoa huo.