KAULI ya Gamondi kuelekea mchezo vs Simba Ngao ya Jamii 2024
KAULI ya Gamondi kuelekea mchezo vs Simba Ngao ya Jamii 2024
KAULI ya Gamondi kuelekea mchezo vs Simba Ngao ya Jamii 2024, Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema kuwa amekiandaa kikosi chake kikamilifu kukabiliana na Simba katika mchezo wa Nusu Fainali wa Ngao ya Jamii kesho Alhamisi uwanja wa Benjamn Mkapa.
Akizungumza katika mkutano na wanahabari kuelekea mchezo huo, Gamondi amesema kuwa mchezo siku zote hauna underdog hivyo watakwenda kucheza kwa tahadhari kubwa wakifahamu huu ni mchezo wa mtoano
Aidha Gamondi amesema kuwa hana taarifa za kutosha kuhusu wapinzani wake Simba ambao wana wachezaji wengi wapya lakini anafahamu mpira ni mchezo wa wazi na ameiandaa timu yake kukabiliana nao katika mazingira yoyote.
“Yaliyopita yamepita, sipendelei kufuatilia sana yaliyopita, huu ni msimu mpya hata wapinzani wetu pia wamebadilika kila kitu kimebadilika, wacha tuone kesho kitatokea nini”
“Tupo imara kiakili na kimwili, tumejianda vya kutosha hakuna tunachohofia, sijapata wasaa mzuri wa kuwatazama wapinzani kwani mechi zake nyingi hazikuoneshwa, lakini hiyo sio changamoto kubwa kwani naanda timu yangu kwa asilimia 75, asilimia 25 ndio natumia kumchunguza mpinzani”
“Hakuna siri kwenye mpira kila kitu lazima kiwe hadharani, kesho ni siku muhimu sana kwani ni mechi ya mtoano, hatupaswi kufanya makosa tunapaswa kuwa makini kwenye kila idara ili kupata matokeo mazuri, naamini mashabiki wetu watajitokeza kwa wingi kwa lengo la kutupa hamasa”
“Naheshimu sana wapinzani wote ninaokutana nao, kesho ni mchezo wa derby hakuna underdog kwenye mchezo huo kwani ni mchezo maalumu sana, najua mpinzani wetu ana timu mpya, wachezaji wapya, wote kwa pamoja watachukua fursa hii kuonesha ubora wao. Kimsingi mchezo huu mizani ipo sawa kwa pande zote 50/50, ni muhimu sana kuendea mchezo huu kwa umakini mkubwa,” alisema Gamondi
Kwa upande wamlinda lango, Aboubakar Khomein amesema kuwa Yanga imejiandaa na mchezo huo kikamilifu, malengo ni kuibuka na ushindi
“Tumejiandaa vizuri sana na tuko tayari, wachezaji wana ari na wote tunawahakikishia kuwa wachezaji tunakwenda kupambana, naamini kesho tutafanya vizuri,” alisema
Tags: KAULI ya Gamondi kuelekea mchezo vs Simba Ngao ya Jamii 2024