RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


LATRA Yatangaza Nauli Treni ya Reli ya Kisasa SGR 2024

Filed in Habari by on 19/07/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

LATRA Yatangaza Nauli Treni ya Reli ya Kisasa SGR 2024

LATRA Yatangaza Nauli Treni ya Reli ya Kisasa SGR 2024, Nauli za Abiria wa Daraja la Kawaida Treni ya SGR, Latra Yatangaza Nauli za Abiria WA Daraja la Kawaida Treni ya SGR.

LATRA Yatangaza Nauli Treni ya Reli ya Kisasa SGR 2024

LATRA Yatangaza Nauli Treni ya Reli ya Kisasa SGR 2024, Nauli za Abiria wa Daraja la Kawaida Treni ya SGR, Latra Yatangaza Nauli za Abiria WA Daraja la Kawaida Treni ya SGR.

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imetangaza taarifa ya maamuzi ya Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini kuhusu nauli za abiria wa daraja la kawaida kwa Treni ya Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam hadi Makutupora.

Nauli hizi ni baada ya kufanyia kazi maombi yaliyoletwa na Shirika
la Reli Tanzania (TRC) na taarifa zilizopokelewa kutoka TRC na wadau wengine.

Kuelekea kuanza kwa safari za SGR Dar es Salaam mpaka Makutupora, masharti
ya kuzingatia kabla ya kuanza kutumika kwa nauli hizi ni kama ifuatavyo:-

  • Mtoa huduma (TRC) kuwa na leseni ya usafirishaji;
  • Kuwa na ithibati ya usalama wa miundombinu ya reli na mabehewa;
  • Kutumia mfumo wa utoaji wa tiketi za kielekroniki;
  • Kuunganisha mfumo wa tiketi za kieletroniki na mifumo ya LATRA;
  • Kukokotoa malipo na utunzaji taarifa za abiria, nauli iliyolipwa, tiketi za kielektroniki zilizotolewa, kodi za Serikali na tozo za kisheria; na,
  • Kuwa na watumishi wa kada muhimu kwa masuala ya ufundi na uendeshaji wa treni ya SGR ikiwa ni pamoja na madereva waliothibitishwa na wahudumu waliosajiliwa na LATRA.

Aidha, nauli hizi ni kwa daraja la kawaida kwa watu wazima na watoto kuanzia umri wa miaka 4 hadi 12 ambapo nauli zitalipwa na abiria kwa kilomita.

Nauli itakayolipwabna mtu mzima na mtoto mwenye umri zaidi ya miaka 12 ni TSH. 69.51 kwa kilomita, na mtoto kuanzia kuanzia miaka 4 hadi 12 atalipia TSH 34.76 kwa kilomita.

Aidha mtoto mwenye umri chini ya miaka minne (4) hatalipa nauli, hata hivyo, taarifa zao na wasafiri wote zitatunzwa kwenye mfumo wa taarifa za abiria wanaosafiri kila siku

Mchanganuo wa nauli hizo kwa daraja la kawaida kulingana na umbali wa vituo kuanzia Dar es Salaam hadi Makutupora kwa watu wazima na watoto wenye umri zaidi ya miaka 12 ni kama ifuatavyo;

BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD PDF YA NAULI ZA ABIRIA WA DARAJA LA KAWAIDA TRENI YA SGR 2024

Vile vile Maeneo ya msingi ya kuzingatiwa na Mtoa Huduma ni pamoja na;

  • Kuweka mfumo wa usimamizi wa utoaji taarifa kwa wasafiri (Passenger Management Information System) na mfumo wa ufuatiliaji wa mwenendo wa
    treni (Train Tracking System);
  • Kuweka nauli za safari ya kituo kwa kituo katika maeneo yanayoonekana na abiria kiurahisi kwa wakati wote;
  • Kuhakikisha uwepo wa huduma bora kwa wateja ikiwemo mazingira ya vituo (stesheni), usafi wa mabehewa, chakula na vinywaji, maji safi na salama,
    mwanga wa kutosha, na kuweka utaratibu wa fidia dhidi ya majanga na upotevu wa mizigo ya abiria; na
  • Kuzingatia vigezo vya usalama wa mabehewa na miundombinu ya reli kwa mujibu wa Sheria, Kanuni za Taratibu zilizopo.

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags: , ,

Comments are closed.