MAGAZETI ya Tanzania Leo Alhamisi August 22-2024
Klabu ya Young Africans ipo kwenye mipango ya kuendelea kukisuka kikosi chake kwa malengo ya kuwa tishio barani Afrika ambapo imepanga kusajili mastaa wawili katika usajili wa dirisha dogo litakaloanza December mwaka huu 2024.
Hayo yamebainishwa na Rais wa Yanga, Mhandisi Hersi Said August 21, 2024 katika mahojiano maalumu na kipindi cha Jana na Leo kinachorushwa na kituo cha redio ya Wasafi FM.
“Bado kikosi chetu hakijakamilika kuwa tishio Afrika, tunafikiria kuongeza wachezaji wawili ambao walikuwa target yetu kwenye dirisha hili kubwa lakini biashara zao hazikukamilika.”
“Dirisha dogo tutarudi kuangalia kama tutaweza kukamilisha sajili zao, wakishafika ndio mtapata majibu maana ya timu kukamilika,” amesema Hersi.
Soma hii pia: FEDHA Watakazopata Washindi wa CAF 2024/2025