MAJINA 103 ya Walioitwa Kwenye Usaili Wilaya ya Ngara July 02-2024
MAJINA 103 ya Walioitwa Kwenye Usaili Wilaya ya Ngara July 02-2024
MAJINA 103 ya Walioitwa Kwenye Usaili Wilaya ya Ngara July 02-2024, Kuitwa Kwenye Usaili Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Leo July 02-2024, Orodha ya Majina ya Walioitwa kwenye Usaili Halmashauri ya Wilaya ya Ngara 02-07-2024.
TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA NGARA 02-07-2024
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 08-07-2024 hadi 09-07-2024 a hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili
wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
- Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.
- Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask)
- Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
- Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga
kura,Kitambulisho cha kazi,Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria. - Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa,kidato cha IV, VI,
Stashahada,Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji. - Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hatiza
matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA
HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI. - Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
- Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
- Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na
Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA) - Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi
vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika. - Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.
- Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa iku ya usaili
- Wasailiwa wote mnajulishwa kuwa hali ya hewa ya wilaya ya Ngara ni baridi hivyo mnashauriwa kuvaa
nguo zinazohimili hali ya hewa ya ubaridi.
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD PDF YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI KUTOKA HALMASHAURI YA WILAYA YA NGARA
Tags: Kuitwa Kwenye Usaili Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Leo July 02-2024, MAJINA 103 ya Walioitwa Kwenye Usaili Wilaya ya Ngara July 02-2024, Orodha ya Majina ya Walioitwa kwenye Usaili Halmashauri ya Wilaya ya Ngara 02-07-2024.