MAJINA 1295 ya Walioitwa Kwenye Usaili Shirika la Posta June 08-2024
MAJINA 1295 ya Walioitwa Kwenye Usaili Shirika la Posta June 08-2024
MAJINA 1295 ya Walioitwa Kwenye Usaili Shirika la Posta June 08-2024, Kuitwa Kwenye Usaili Shirika la Posta Tanzania June 08-2024, Orodha ya Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Shirika la Posta Tanzania Leo tarehe 08-2024, Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Posta Leo tarehe 8 June 2024.
Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania anapenda kuwataarifu waombaji wote wanafasi mbalimbali za kazi kufika kwa ajili ya usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia
tarehe 15/06/2024 hadi 21/06/2024 hatimaye kuajiriwa waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.
Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
- Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye ratiba ya tangazo hili muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila kada;
- Kila msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
- Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura,Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia, Hati
ya kusafiria au barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji unachotoka; - Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa,kidato cha IV, VI, Astashahada, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji;
- Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips)
HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI; - Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi;
- Kila msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili;
- Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwabna kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA);
- Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa
kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi; - Wasailiwa wote mnaelekezwa kufika eneo la usaili dakika arobaini (40) kabla ya muda wa Usaili uliopangwa kuanza; na
- Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi
zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD PDF YA MAJINA 1295 YA WALIOITWA KWENYE USAILI SHIRIKA LA POSTA TANZANIA LEO JUNE 08-2024
Kihistoria asili ya mawasiliano duniani yalianzia katika mfumo wa kiposta, ambapo watu na jamii mbalimbali ziliwasiliana kwa njia ya maneno ya mdomo au kwa maandishi kwa kutumia matarishi, punda, ngamia, wapanda farasi au watembea kwa miguu. Hawa walipokezana taarifa katika vituo vilivyoteuliwa kwenye njia kuu. Katika baadhi ya jamii za Kiafrika ikiwemo Tanzania, ngoma pia zilitumika katika kupeana taarifa.
Mfumo huu uliwanufaisha zaidi wafalme na watawala wa kijadi ambao dhamira yao kuu ilikuwa kuwarahisishia uendeshaji wa shughuli za kiutawala hususan katika kuhakisha kuwa maelekezo, amri na miongozo yao inawafikia watawaliwa.
Mfumo huu ulikuwa ukiboreshwa sanjari na historia ya maendeleo ya binadamu na hadi kufikia karne ya kumi na nane huduma za Posta zikawa zinasimamiwa katika mifumo ya kitaasisi katika ngazi za kitaifa na kimataifa. Mwaka 1874 ulianzishwa Umoja wa Posta Duniani (UPU) Umoja huu ambao makao yake makuu yako Mjini Berne – Uswizi ikiwa ni taasisi ya pili ya kimataifa kuanzishwa baada ya Umoja wa Mawasiliano ya Simu (ITU) mwaka 1865. UPU ni Shirika tanzu la Umoja wa Mataifa (UN) lenye jukumu la kusimamia maendeleo ya shughuli za Posta Kimataifa.
HISTORIA YA POSTA KABLA YA UHURU WA TANGANYIKA
Huduma za Posta kama taasisi zilianzishwa nchini na Serikali ya kikoloni ya Ujerumani ambayo ilitawala kwa pamoja nchi za Tanganyika, Rwanda na Burundi.
Makao Makuu ya Posta kwa nchi zote hizi yakiwa katika jengo la Posta ya Sokoine (Posta ya Zamani) jijini Dar es Salaam. Huduma ya kwanza ya barua iliyobandikwa stempu ilianzishwa hapa nchini mwaka 1893. Barua hizo zilitumwa kwa kutumia matarishi waliokuwa wanatembea kwa miguu umbali mrefu kutoka Makao Makuu ya Wilaya hadi Majimbo. Huduma ya treni kati ya Dar es Salaam hadi Kigoma na baadae hadi Mwanza na Arusha iliboresha mtandao wa huduma za Posta nchini.
Tags: Kuitwa Kwenye Usaili Shirika la Posta Tanzania June 08-2024, MAJINA 1295 ya Walioitwa Kwenye Usaili Shirika la Posta June 08-2024, Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Posta Leo tarehe 8 June 2024., Orodha ya Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Shirika la Posta Tanzania Leo tarehe 08-2024