MAJUKUMU ya Afisa Mtendaji wa Kata
MAJUKUMU ya Afisa Mtendaji wa Kata
MAJUKUMU ya Afisa Mtendaji wa Kata,Majukumu ya Afisa Mtendaji wa Kata Tanzania, Yafahamu Majukumu ya Afisa Mtendaji wa Kata Tanzania.
- Atakuwa Mtendaji Mkuu wa Kata na kiungo cha Uongozi kwa Idara zote katika kata na atashughulikia masuala yote ya kata.
- Atakuwa Mhamasishaji mkuu wa Umma katika mikakati mbalimbali ya uzalishaji, mali, kuondoa njaa na Umasikini.
- Atakuwa ni Katibu wa kamati ya maendeleo ya kata.
- Ataratibu na kusimamia upangaji wa shughuli za maendeleo ya kata, vijiji na vitongoji.
- Atatafsiri sera na kusimamia utekelezaji wa sheria ndogondogo katika Kata yake.Atamsaidia Mkurugenzi Kuratibuna kusimamia shughuli za Uchaguzi katika Kata.
- Kumsaidia na kumwakilisha Mkurugenzi katika kusimamia maendeleo ya eneo lake.
- Kusimamia utendaji kazi wa wataalamu na watendaji wengine katika ngazi ya Kata.
- Kuratibu na kuandaa taarifa za utekelezaji na kuziwasilisha kwa mkurugenzi na nakala kwa Katibu Tarafa.
- Atakuwa mwenyekiti katika vikao vya vinavyowahusisha wataalamu na watendaji wa vjiji, na NGO’S katika kata yake.
- Atakuwa Msimamizi na mratibu wa takwimu zote zinazokusanywa katika vijiji, vitongoji, na kata yake.