RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


MAMBO ya Kuzingatia wakati wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura 2024

Filed in Ajira, Habari by on 30/06/2024

MAMBO ya Kuzingatia wakati wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura 2024

MAMBO ya Kuzingatia wakati wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura 2024

MAMBO ya Kuzingatia wakati wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura 2024

MAMBO ya Kuzingatia wakati wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura 2024,Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi inawatangazia wananchi wote kuwa Uzinduzi wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Awamu ya Kwanza utafanyika Mkoa wa Kigoma tarehe 20 Julai, 2024.

Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo atakuwa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (MB).Mara baada ya uzinduzi, zoezi la Uboreshaji wa Daftari litaendelea Mkoani Kigoma hadi tarehe 07 Julai, 2024.

SIKU: Uboreshaji utafanyika kuanzia tarehe 20 Julai, 2024.

VITUO: Uboreshaji utafanyika katika vituo vilivyomo katika Mitaa, vijiji na Vitongoji.

MUDA: Vituo vitafunguliwa saa 2:00 Asubuhi na kufungwa saa 12:00 Jioni.

Uboreshaji utahusisha: –

  • Kuandikisha Wapiga Kura wapya ambao ni raia wa Tanzania waliotimiza umri wa Miaka 18 na zaidi na hawakuwahi kuandikishwa hapo awali.
  • Kuandikisha Wapiga kura ambao watakuwa wametimiza umri wa miaka 18 siku ya tarehe ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.
  • Kuboresha taarifa za wapiga kura waliohama kutoka eneo moja kwenda eneo lingine la kiuchaguzi.
  • Kutoa kadi mpya kwa wapiga kura ambao kadi zao zimepotea au kuharibika.
  • Kuboresha au kurekebisha taarifa za wapiga kura.
  • Aidha,Wapiga kura wanaotaka kuboresha taarifa zao na wanaohama kituo cha kupigia kura au vyote viwili wanaweza kuanzisha mchakato wa kuboresha kwa kujaza fomu maalum kwa njia ya mtandao kupitia anuwani ya ovrs.inec.go.tz kwa kujaza namba ya kitambulisho cha Taifa, namba ya kadi ya mpiga kura, namba ya simu ya mpiga kura na jina la kata kisha watapokea ujumbe wenye namba ya utambulisho (token number) ambayo wataenda nayo kituo cha kujiandikisha ili kukamilisha taratibu na kupata kadi ya mpiga kura.

MAMBO YA KUZINGATIA

  • Mwananchi anatakiwa kupanga mstari akiwa kituoni na kusubiri hadi zamu yake ya kuandikishwa itakapowadia.
  • Watu wenye mahitaji maalumu kama vile wazee, wagonjwa, watu wenye ulemavu, wajawazito na akina mama wenye watoto wachanga watakaokwenda nao kituoni watapewa kipaumbele.
  • Mwananchi atakapofika kituo cha kujiandikisha atachukuliwa alama za vidole vyote kumi vya mikono na kupigwa picha na kisha kupewa kadi yake mpya hapo hapo kituoni
  • Ni muhimu kujiandikisha sasa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ili uweze kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 na chaguzi zijazo
  • Zoezi hili halitawahusu wapiga kura ambao waliandikishwa awali, hawajahama maeneo yao ya kiuchaguzi na wana kadi zao za mpiga kura.

MAMBO ya Kuzingatia wakati wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura 2024

Tags:

Comments are closed.