RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


MIFUMO Miwili Kurahisisha Maboresho ya Daftari la Kudumu la Wapiga Kura 2024

Filed in Habari by on 30/06/2024

MIFUMO Miwili Kurahisisha Maboresho ya Daftari la Kudumu la Wapiga Kura 2024

MIFUMO Miwili Kurahisisha Maboresho ya Daftari la Kudumu la Wapiga Kura 2024

MIFUMO Miwili Kurahisisha Maboresho ya Daftari la Kudumu la Wapiga Kura 2024

MIFUMO Miwili Kurahisisha Maboresho ya Daftari la Kudumu la Wapiga Kura 2024,Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa anatarajiwa kuzindua rasmi zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura nchini July 20-2024.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele uzinduzi huo utafanyika rasmi mkoani Kigoma.

Vile vile, siku ya uzinduzi ndiyo siku ambayo pia uboreshaji utaanza katika Mkoa wa Kigoma, Katavi, Tabora, Kagera na Geita na baadaye mikoa mingine.

Ili kutekeleza jukumu hilo kwa ufanisi, tume inatarajia kutekeleza zoezi hilo katika awamu ya kwanza kupitia mizunguko 13 kadri itakavyokuwa ikitoa ratiba.

Aidha, Kupitia Mikutano na wadau mbalimbali iliyoanza Juni 7, 2024 ambapo Tume imekuwa ikikutana nao wakiwemo Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, viongozi wa Tume wamebainisha kuwa,

Katika Uboreshaji huo kutakuwa na mifumo miwili ukiwemo Mfumo Mkuu wa VRS (Voter Registration System) na Mfumo Saidizi wa OVRS (Online Voter Registration System).

VRS ni mfumo ambao umekuwa ukitumika katika mazoezi ya Uboreshaji wa Daftari uliotangulia ikiwemo mwaka 2015 na 2020.

Huku, OVRS ni mfumo ambao Tume imeuanzisha kwa lengo la kurahisisha Utoaji huduma kwa Wananchi kwa njia ya Mtandao.

Kwa mujibu wa INEC, Mifumo yote miwili itahusisha Matumizi ya Fomu tatu za uandikishaji kama ilivyokuwa katika mazoezi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura miaka ya 2014/15 na 2019/20.

Fomu Namba 1 itahusika kuandikisha wapiga kura wapya, Fomu Namba 5A ni kwa wanaoboresha taarifa zao, wanaohama vituo, waliopoteza kadi au kadi zao kuharibika.

Wakati huo huo, Fomu Namba 5B ni kwa ajili ya kuondoa taarifa za wapiga kura waliopoteza sifa za kuwepo katika Daftari la Wapiga Kura nchini.

INEC imebainisha kuwa, Mifumo yote miwili inahusisha matumizi ya Namba ya Utambulisho wa Taifa (NIN) ambayo huwa inatolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Aidha, Mifumo hiyo ya uandikishaji ya INEC inaweza kuvuta taarifa za NIDA iwapo mpira kura atakuwa na NIN, hivyo kurahisisha zoezi la uandikishaji ingawa namba hiyo si hitaji la lazima ili mpiga kura kujiandikisha.

Akiwasilisha mada yake kwenye Mikutano hiyo, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw.Ramadhani Kailima amesema, kuwa Uboreshaji wa Daftari pamoja na mambo mengine utahusu kuandikisha wapiga kura wapya ambao ni raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na zaidi na watakaotimiza umri huo ifikapo tarehe ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Ameongeza kuwa zoezi hilo pia Iitatoa fursa kwa wapiga kura waliopo kwenye daftari na ambao wamehama, waweze kuhamisha taarifa zao kutoka kata au jimbo walioandikishwa awali.


TUME YAKAMILISHA MAANDALIZI YA UBORESHAJI WA DAFTARI IKIWEMO KUNUNUA BVR KITS 6,000

Katika hatua nyingine, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imesema kuwa imekamilisha maandalizi muhimu kwaajili ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ikiwa ni pamoja na ununuzi wa vifaa vya uandikishaji vinavyojumuisha BVR Kits 6,000.

Hayo yamebainishwa tarehe 10 Juni, 2024 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima, R. K wakati akiwasilisha mada kwenye mkutano wa Tume na Viongozi wa Dini.

Mkutano huo umefanyika sambamba na mkutano wa Tume na Taasisi na Asasi za kiraia ikiwa ni muendelezo wa utaratibu wa Tume wa kuwashirikisha wadau wa uchaguzi kabla ya kuanza rasmi kwa uboreshaji wa Daftari.

Bw. Kailima amesema kuwa BVR Kits hizo zitatumia vishkwambi kuchukua taarifa za wapiga kura ikiwemo picha, saini na alama za vidole.

“BVR Kits za sasa zinatumia mfumo endeshi wa android na uzito wake ni kilogramu 18, awali zilikuwa zinatumia mfumo endeshi wa window na uzito wa kilogramu 35,” amesema Bw. Kailima.

Amesema Mfumo wa Uandikishaji wa Wapiga Kura (Voters Registration System-VRS) umefanyiwa usanifu na kuboreshwa ili kukidhi aina ya BVR Kits za sasa ambazo zinatumia programu endeshi ya android.

Wakati akifungua mkutano huo, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele amesema, BRV Kits hizo zitakuwa rahisi kubeba na kufanya zoezi la Uboreshaji wa Daftari kuwa rahisi haswa kwenye maeneo ya Vijijini ambapo Watendaji hulazimika kubeba vifaa kwa umbali mrefu.

“Amesema mfumo wa teknolojia hii ya BVR hutumika katika kumtambua mtu na kumtofautisha na mwingine. Uandikishaji huu wa wapiga kura utahusisha uchukuaji wa alama za vidole vya mikono, picha na saini na kuhifadhiwa kwenye kanzidata ya wapiga kura,” amesema.

Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utazinduliwa mkoani Kigoma tarehe 01 Julai, 2024 na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (MB).

Tags:

Comments (1)

Trackback URL | Comments RSS Feed

  1. Mwanza mbona bado majina ya walio itwa kwenye usaili