MO Dewji Tajiri namba 12 Barani Africa 2024
MO Dewji Tajiri namba 12 Barani Africa 2024
MO Dewji Tajiri namba 12 Barani Africa 2024,Utajiri wa mo dewji Afrika 2024, Utajiri wa mo dewji Afrika Mashariki 2024, Utajiri wa Mo Dewji Forbes, Utajiri wa mo dewji kwa fedha za kitanzania, Tajiri namba moja tanzania, Mo dewji na ronaldo nani tajiri, Utajiri wa Mo Dewji 2024.
Mfanyabiashara Maarufu nchini Tanzania na Rais wa heshima wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji (Mo) ametajwa na Jarida la Forbes kuwa tajiri namba 12 barani Afrika na Bilionea kijana zaidi kwa kipindi cha miaka 10 Mfululizo
Kwa mujibu wa jarida hilo Mashuhuri ambalo hufuatilia ukwasi wa watu, ndani ya kipindi cha miaka miwili iliyopita Mohammed Dewji ‘Mo’ amepanda kiutajiri Barani Afrika kutoka nafasi ya 15 hadi 12.
Mbali na kupanda kiutajiri, Mfanyabiashara huyo anayemiliki Kampuni ya Mohammed Enterprises Ltd (METL), utajiri wake umepanda kutoka Dola za Marekani 1.5 Bilioni (Sh3.77 trilioni) mwaka uliopita hadi Dola 1.8 bilioni (Sh4.52 trilioni) jambo linalomfanya kuwa tajiri namba moja ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Ripoti inaonyesha kwa ujumla ukwasi wa mabilionea 20 wanaoongoza Afrika uliongezeka kwa Dola milioni 900 (Sh2.26 trilioni) na kufika Dola bilioni 82.4 (Sh207.23 trilioni) mwaka 2024.
Upimaji wa ukwasi wa watu uliofanywa na Forbes uliangalia gharama halisi kwenye masoko ya mitaji na viwango vya kubadilishia fedha vilivyopo sokoni hadi Januari 8, 2024.
METL ambayo imejikita kwenye biashara mbalimbali zikiwamo za vyakula na vinywaji, ikimiliki viwanda kadhaa ndani na nje ya Tanzania, imeajiri zaidi ya wafanyakazi 40,000.
Katika orodha hiyo, bilionea wa Nigeria, Aliko Dangote aliyejikita kwenye viwanda vikiwamo vya saruji anashika nafasi ya kwanza akiwa na utajiri wa Dola bilioni 13.9 bilioni za Marekani akifuatiwa na Johann Rupert, nafasi ya pili akiwa na utajiri wa Dola bilioni 10.1 za Marekani.
Nafasi ya tatu inashikwa na familia ya Nicky Oppenheimer yenye utajiri wa Dola bilioni 9.4, huku Nassef Sawiris akishika nafasi ya nne akiwa na utajiri wa Dola bilioni 9.4. Sehemu kubwa ya utajiri wa Nassef unatokana na uwekezaji kwenye biashara ya madini.
Mwingine aliye kwenye orodha ya mabilionea 20 barani Afrika ni Mike Adenuga mwenye utajiri wa Dola bilioni 6.9 akishika nafasi ya tano, huku Abdulsamad Rabiu akishika nafasi ya sita akiwa na utajiri wa Dola bilioni 5.9.
Naguib Sawiris, aliyejikita kwenye biashara ya mawasiliano anashika nafasi ya saba akiwa na utajiri wa Dola bilioni 3.8. Mohamed Mansour anashika nafasi ya nane akiwa na utajiri wa Dola bilioni 3.2 bilioni. Tajiri namba tisa kwa mujibu wa Forbes ni Koos Bekker, anayejikita kwenye biashara za mawasiliano na burudani akiwa na utajiri wa Dola bilioni 2.7.
Bilionea wa Afrika Kusini, Patrice Motsepe anashika nafasi ya tisa pia akiwa na utajiri wa Dola bilioni 2.7. Bilionea huyu ambaye amejikita kwenye biashara za madini, pia ni mmiliki wa klabu ya Mamelod Sundown ya Afrika Kusini.
Motsepe kwa sasa ndiye Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) akiwa amefanya uwekezaji mkubwa kwenye soka nchini Afrika Kusini.
Nafasi ya 11 kwenye orodha hiyo inashikiliwa na Familia ya Issad Rebrab akiwa na utajiri wenye thamani ya Dola bilioni 2.5 akiwekeza zaidi kwenye biashara ya vyakula na vinywaji.
Mfanyabiashara na mwekezaji kwenye klabu ya Simba, Mohammed Dewji (Mo) anashika nafasi ya 12 kwenye orodha ya mabilionea barani Afrika akiwa na utajiri wa Dola bilioni 1.8 bilioni. Kwa sasa ni Rais wa Heshima wa Klabu ya Simba.
Katika kampuni za METL, licha ya kuajiri Watanzania wengi, Mo pia amekuwa sehemu ya msaada kwa jamii kupitia Taasisi ya Mo Foundation iliyojikita kusaidia vijana wa Kitanzania kutimiza ndoto zao kielimu.
Mo Foundation imekuwa ikitoa ufadhili wa masomo kila mwaka kwa wanafunzi wanaofanya vizuri kusoma vyuo vya ndani na nje ya Tanzania.
Katika orodha hiyo, Strive Masiyiwa anashika nafasi ya 13 akiwa na utajiri wa Dola bilioni 1.8, Aziz Akhannouch anashika nafasi ya 14 akiwa na Dola bilioni 1.7.
Nafasi ya 15 inashikiliwa na Othman Benjelloun akiwa na Dola bilioni 1.4, Youssef Mansour anashika nafasi ya 16 akiwa na Dola bilioni 1.3, Yasseen Mansour yuko nafasi ya 17 akiwa na ukwasi wa Dola bilioni 1.2, huku Christoffel Wiese akiwa na utajiri wa Dola bilioni 1.2 katika nafasi ya 18.
Wengine ni Michiel Le Roux katika nafasi ya 19 akiwa na utajiri wa Dola bilioni 1.1 na Femi Otedola anafunga dimba la 20 bora akiwa na utajiri wa Dola bilioni 1.1.
Rank | Name | Net Worth | Age | |
---|---|---|---|---|
#1 | Aliko Dangote | $13.9 B | 66 | |
#2 | Johann Rupert | $10.1 B | 73 | |
#3 | Nicky Oppenheimer | $9.4 B | 78 | |
#4 | Nassef Sawiris | $8.7 B | 63 | |
#5 | Mike Adenuga | $6.9 B | 70 | |
#6 | Abdulsamad Rabiu | $5.9 B | 63 | |
#7 | Naguib Sawiris | $3.8 B | 69 | |
#8 | Mohamed Mansour | $3.2 B | 76 | |
#9 | Koos Bekker | $2.7 B | 71 | |
#9 | Patrice Motsepe | $2.7 B | 61 |
#11 | Issad Rebrab | $2.5 B | 80 | |
#12 | Mohammed Dewji | $1.8 B | 48 | |
#12 | Strive Masiyiwa | $1.8 B | 62 | |
#14 | Aziz Akhannouch | $1.7 B | 63 | |
#15 | Othman Benjelloun | $1.4 B | 91 | |
#16 | Youssef Mansour | $1.3 B | 78 | |
#17 | Yasseen Mansour | $1.2 B | 62 | |
#17 | Christoffel Wiese | $1.2 B | 82 | |
#19 | Michiel Le Roux | $1.1 B | 74 | |
#19 | Femi Otedola | $1.1 B | 61 |
Orodha ya matajiri 100 duniani, Matajiri 10 Tanzania Forbes, Tajiri namba moja afrika, Bakhresa ni tajiri wangapi africa, Matajiri 10 Tanzania 2024, Matajiri afrika 2024 map, Top 20 richest in Africa, Top 100 richest people in Africa, Top 50 richest people in Africa, Richest man in Africa 2024, Who is the top 10 richest in Africa, Youngest richest man in Africa, Richest woman in Africa, Richest president in Africa, The richest country in Africa, Aliko Dangote net worth, Top 10 richest country in Africa.
PIA UNAWEZA KUSOMA👇
- MATOKEO Ya Darasa la Nne 2023/2024
- MATOKEO ya Kidato Cha Pili 2023/2024
- JINSI ya Kuangalia Matokeo Kidato Cha Nne 2023/2024
- ADA za Lipa kwa Airtel Mitandao Yote
- Ada mpya za M-Pesa 2023/2024
- TETESI Za Usajili Yanga SC Dirisha Dogo 2023/2024
- Ada/makato ya Lipa kwa M-pesa, Lipa kwa Simu
- TETESI Za Usajili Simba SC Dirisha Dogo 2023/2024
- ORODHA ya Vilabu Bora Afrika November 2023 (IFFHS Club Ranking)
- MSIMAMO Kundi D CAF Champions League 2023/2024
- MSIMAMO Wa Kundi B CAF Champions League Standings 2023/2024
- DOWNLOAD | NYIMBO ZA TENZI ZA ROHONI SWAHILI MIX
- MSIMAMO NBC Premier League 2023/2024
- WAFUNGAJI Wanaoongoza Magoli NBC Premier League 2023/2024
- KIKOSI cha Yanga SC msimu wa 2023/2024
- RATIBA Kamili Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania 2023/2024
- RATIBA Kamili ya Ligi Kuu ya NBC 2023/2024
- RATIBA ya Mechi za Simba SC Ligi Kuu ya NBC 2023/2024
- RATIBA ya Mechi za Yanga SC Ligi Kuu ya NBC 2023/2024
- RATIBA Kamili ya Ligi Kuu ya England (EPL 2023/2024)
- KIKOSI cha Simba SC msimu wa 2023/2024
Tags: Mo dewji na ronaldo nani tajiri, MO Dewji Tajiri namba 12 Barani Africa 2024, Tajiri namba moja tanzania, Utajiri wa Mo Dewji 2024., Utajiri wa mo dewji Afrika 2024, Utajiri wa mo dewji Afrika Mashariki 2024, Utajiri wa Mo Dewji Forbes, Utajiri wa mo dewji kwa fedha za kitanzania