RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI 10 za Kazi Wilaya ya Chunya July 09-2024

Filed in Ajira by on 09/07/2024

NAFASI 10 za Kazi Wilaya ya Chunya July 09-2024

NAFASI 10 za Kazi Wilaya ya Chunya July 09-2024

NAFASI 10 za Kazi Wilaya ya Chunya July 09-2024

NAFASI 10 za Kazi Wilaya ya Chunya July 09-2024, Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Chunya 09-07-2024,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya amepokea kibali cha Ajira Mpya kwa Ikama ya mwaka 2023/2024 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chenye Kumb. Namba FA.97/288/01/09 ya tarehe 25/06/2024.

Hivyo Watanzania wote wenye sifa wanatangaziwa kutuma maombi ya kazi kwabnafasi zifuatazo:-

✅DEREVA II – NAFASI 1

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;
  • Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kazi;
  • Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari;
  • Kutunza na kuandika daftari la safari “log book’’ kwa safari zote;
  • Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali;
  • Kufanya usafi wa gari; na
  • Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.

SIFA ZA MWOMBAJI:

Awe amehitimu kidato cha nne (IV) na kupata cheti cha mtihani wa kidato cha Nne (IV). Awe na leseni ya daraja la ‘C’ au ‘E’ ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingazia Ngazi ya Mishahara ya Serikali TGS –B
1.2

✅MWANDISHI MWENDESHA OFISI II – NAFASI 2

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za siri;
  • Kupokea wageni na kuwasikiliza shida zao, na kuwaelekeza sehemu
    wanapoweza kusaidiwa;
  • Kutunza taarifa na kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine;
  • Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa
    majukumu ya kazi;
  • Kupokea majalada na kusambaza kwa maofisa walio katika Idara/Kitengo/ Sehemu husika;
  • Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika;
  • Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali ; na
  • Kuandaa orodha ya mahitaji ya ofisi.

SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amahitimu kidato cha nne (IV) au Kidato cha Sita (VI) na kupata cheti cha Mtihani wa Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI). Awe na Stashahada (Diploma) ya Uhazili au Cheti cha NTA level 6 ya uhazili kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

Aidha, awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na Awe amepata mafunzo ya programu za kompyuta za ofisi kama vile: Word, Excel, Powerpoint, Internet, Email na Publisher.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingazia Ngazi ya Mishahara ya Serikali TGS –C

✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II- NAFASI 2

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kuorodhesha barua zinazoingia masjala kwenye rejista (incoming
    correspondence register);
  • Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya taasisi kwenye rejista (outgoing
    correspondence register);
  • Kusambaza majalada kwa watendaji (Action Officers);
  • Kupokea majalada yanayorudi masjala toka kwa watendaji (Action
    Officers);
  • Kutafuta kumbukumbu /nyaraka/majalada yanayohitajika na watendaji (Action Officers);
  • Kurudisha majalada kwenye shubaka/kabati la majalada (ranks/filling cabinets) au mahali pengine yanapohifadhiwa;
  • Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya taasisi ( File tracking);

SIFA ZA MWOMBAJI:
Awe amehitimu kidato cha nne (IV) au kidato cha sita (IV) na kupata cheti cha mtihani wa Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI). Awe amehitimu mafunzo ya Stashahada/Diploma (NTA level 6) katika fani ya Masjala kutoka vyuo vinavotambuliwa na serikali, pia awe na ujuzi wa kompyuta.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingazia Ngazi ya Mishahara ya Serikali TGS –C

NAFASI 10 za Kazi Wilaya ya Chunya July 09-2024✅MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III – NAFASI 5

  • MAJUKUMU YA KAZIAfisa masuuli na Mtendaji mkuu wa Serikali ya kijiji;
  • Kusimamia Ulinzi na Usalama wa raia na mali zao ,Kuwa mlinzi wa
    Amani na usimamizi wa Utawala Bora katiaka kijiji;
  • Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya
    maendeleo ya kijiji;
  • Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji;
  • Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu;
  • Kuandaa Taarifa za Utekelezaji wa kazi katika eneo lake na
    kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya
    kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali;
  • Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalamu katika kijiji;
  • Kusimamia, Kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyarakabza Kijiji;
  • Mwenyekiti wa kikao cha Wataalamu waliopo katika kijiji;
  • Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi;
  • Kusimamia utungaji wa Sheria ndogo za kijiji; na
  • Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.
  • Pamoja na kazi nyingine utakazopangiwa na Mwajiri wako.

SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu elimu ya kidato cha Nne (IV) au Sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya
Astashahada (Cheti) NTA Level 5 katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha , Maendeleo ya jamii na Sayansi ya Jamii kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingazia Ngazi ya Mishahara ya Serikali TGS –B

MASHARTI YA JUMLA KWA MUOMBAJI

  • Waombaji wote wawe raia wa Tanzania na wenye umri kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini;
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa
    kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma;
  • Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (Detail Curriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya
    Barua pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika;
  • Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
    katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi ya kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo;
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na Vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia
    sifa za kazi husika.
  • Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates – Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI – Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaalumab(Proffessional Certificate from Respective Boards)
  • “Testmonial” “Provisioinal Result”,”Statement of result”, hati ya matokeo ya Kidato
    cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
    HAVITAKUBALIWA.
  • Wapombaji waliosoma nje Nchi wahakikishe vyeti vyao vinahakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA NA NACTE).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali kutoka kwa Katibu Mkuu KiongoziWaombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 21 Julai, 2024

MUHIMU: Kumbuka kuambatanisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:-
MKURUGENZI MTENDAJI
HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA
S. L. P 73
CHUNYA

Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment
Portal) kupitia anauani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ . Anuani hii inapatikana pia kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’.

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIKIWA.

DONWLOAD PDF DOCUMENT

Tags:

Comments are closed.