RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI 12 za Kazi Wilaya Ya Mkinga July 18-2024

Filed in Ajira by on 18/07/2024

NAFASI 12 za Kazi Wilaya Ya Mkinga July 18-2024

NAFASI 12 za Kazi Wilaya Ya Mkinga July 18-2024

NAFASI 12 za Kazi Wilaya Ya Mkinga July 18-2024

NAFASI 12 za Kazi Wilaya Ya Mkinga July 18-2024,Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Mkinga 18-07-2024,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga amepokea kibali cha Ajira mpya kwa ikama ya mwaka 2023/2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye Kumb.Na.FA.97/288/01/09 cha tarehe 25/06/2024.

Hivyo Watanzania wote wenye sifa wanatangaziwa kutuma maombi ya kazi kwa nafasi zifuatazo:-

✅DEREVA II – NAFASI 05

MAJUKUMU YA KAZI YA DEREVA II

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;
  • Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi;
  • Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari;
  • Kutunza na kuandika daftari la safari “log book” kwa safari zote;
  • Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali;
  • Kufanya usafi wa Gari; na
  • Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.

SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu kidato cha nne (IV) na kupata Cheti cha Mtihani wa Kidato cha Nne (IV). Awe na leseni daraja ‘C’ au “E” ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali, Awe amehudhuria
mafunzo ya msingi ya Uendeshaji Magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS – B

✅WANDISHI MWENDESHA OFISI II – NAFASI 02

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za Siri;
  • Kupokea wageni na kuwasikiliza shida zao na kuwaeleza wanapoweza kusaidiwa;
  • Kutunza taarifa za kumbukumbu ya matukio, miadi, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba za kazi zingine;
  • Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi;
  • Kupokea majalada na kusambaza kwa maofisa walio katika Idara/Kitengo/Sehemu husika;
  • Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika;
  • Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali; na
  • Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya Ofisi.

SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI) na kupata Cheti cha Mtihani wa Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI). Awe na Stashahada (Diploma) ya Uhazili au Cheti cha NTA level 6 ya Uhazili kutokakatia Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali. Awe
amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na. Awe amepata mafunzo ya programu za Kompyuta za ofisi kama vile Word, Excel, Power point, Internet, E-mail na Publisher.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS – C

✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – NAFASI 03

KAZI NA MAJUKUMU YA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II

  • Kuorodhesha barua zinazoingia masjala kwenye Regista (Incomming Correspondence
    Register);
  • Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya Taasisi (Outgoing Correspondence Register);
  • Kusambaza majalada kwa watendaji (Action Officers);
  • Kupokea majalada yanayorudi masjala kutoka kwa watendaji;
  • Kutafuta kumbukumbu/Nyaraka au majalada yanayohitajika na watendaji;
  • Kurudisha majalada kwenye shubaka/kabati la majalada (Racks/Filling Cabinets) au
    Mahali Pengine yanapohifadhiwa; na
  • Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani na nje ya Taasisi (File tracking).

SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI) aliyehitimu Stashahada (NTA level 6) katika fani ya Masjala kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, mwenye ujuzi wa Kompyuta.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS – C

✅MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA III – NAFASI 02

MAJUKUMU YA KAZI

  • Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa serikali ya Kijij
  • Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao, kuwa mlinzi wa amani na msimamizi wa utawala bora katika kijiji;
  • Kuratibu na kusimamia upangaji wa mipango ya maendeleo ya kijiji;
  • Katibu wa mikutano na kamati zote za Halmashauri ya kijiji;
  • Kutafsiri na Kusimamia Sera, Sheria na Taratibu;
  • Kuandaa taarifa ya utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongezanuzalishaji mali;
  • Kiongozi wa wakuu wa vitengo vya klitaalam katika kijiji;
  • Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za kijiji;
  • Mwenyekiti wa kikao cha wataalam waliopo katika kijiji;
  • Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi; na
  • Kusimamia utungaji wa Sheria Ndogo za kijiji;

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye Elimu ya kidato cha Nne(IV) au Sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti katika moja ya fani zifuatazo: Utawala,Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo Cha Serikali za Mitaa au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS – B

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini;
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa
    kwa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi waUmma
  • Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (DetailCurriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya
    Barua Pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
  • Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia Sifa zakuingilia
    katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi yanafasi ya kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo.
  • Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detail C.V) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika;
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/ Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale waliofikia
    kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi
    husika.
    Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates, – Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, – Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Professional Certificate from Respective
    Boards);
  • Testmonial“, ‘‘Provisional Results“, “Statement of results“, hati ya matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
    HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika
    Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 31 Julai, 2024.

MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa: –
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya Mkinga,
S.L.P. 6005,
TANGA.

Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya
Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).

Maombi yatakayowasiIishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

DONWLOAD PDF DOCUMENT

Tags:

Comments are closed.