RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI 13 za Kazi Wilaya ya Ngorongoro July 2024

Filed in Ajira by on 21/07/2024

NAFASI 13 za Kazi Wilaya ya Ngorongoro July 2024

NAFASI 13 za Kazi Wilaya ya Ngorongoro July 2024

NAFASI 13 za Kazi Wilaya ya Ngorongoro July 2024

NAFASI 13 za Kazi Wilaya ya Ngorongoro July 2024,Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro 21-07-2024,Kufuatia kutolewa kwa Kibali cha Ajira mpya chenye Kumb. Na. FA.97/288/01/09 cha tarehe 25 Juni, 2024 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro anawatangazia nafasi za kazi Watanzania wenye sifa na uwezo ya kujaza nafasi zifuatazo;-

✅MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA III – (NAFASI 10)

MAJUKUMU YA MTENDAJI WA KIJIJI

  • Afisa Masuuli na Mtendaji mkuu wa serikali ya kijiji
  • Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao, kuwa mlinzi wa amani na msimamizi wa utawala bora katika kijiji
  • Kuratibu na kusimamia upangaji wa mipango ya maendeleo ya kijiji
  • Katibu wa mikutano na kamati zote za Halmashauri ya kijiji;
  • Kutafsiri na Kusimamia Sera, Sheria na Taratibu;
  • Kuandaa taarifa ya utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini
    na kuongeza uzalishaji mali;
  • Kiongozi wa wakuu wa vitengo vya kitaalama katika kijiji;
    viii.Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za kijiji;
  • Mwenyekiti wa kikao cha wataalam waliopo katika kijiji;
  • Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi;
  • Kusimamia utungaji wa Sheria Ndogo za kijiji; na
  • Atawajibika kwa Mtendaji Mkuu wa Kata.
  • Pamoja na kazi nyingine utakazopangiwa na Mwajiri wake.

SIFA ZA KUAJIRIWA
Waombaji wanatakiwa wawe wenye Elimu ya Kidato cha Nne (Form IV) au Sita (Form Six) aliyehitimu astashahada/cheti katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu
ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B.

✅DEREVA DARAJA LA II – (NAFASI 3)

MAJUKUMU YA DEREVA

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
  • Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
  • Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
  • Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
  • Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari naKufanya usafi wa gari

SIFA ZA KUAJIRIWA
Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Sita (VI), Awe na Leseni ya Daraja la C au E ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Cource) yanayotolewa na chuo cha VETA au NIT au Chuo kingine
kinachotambulika na Serikali.

MSHAHARA; Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B 1.

MASHARTI YA JUMLA YA WAOMBAJI WOTE

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini;
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi waUmma
  • Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (DetailCurriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya Barua Pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
  • Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia Sifa zakuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi yanafasi ya kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo.
  • Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detail C.V) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini
    (referees) watatu wa kuaminika;
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/ Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale
    waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
    Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates, – Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, – Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Professional Certificate from Respective Boards);
  • “Testmonial“, ‘‘Provisional Results“, “Statement of results“, hati ya matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
    HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo
    katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

Mwisho wa kutuma maombi ya kazi hizi ni tarehe 01 Agosti, 2024.

MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:-
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya Ngorongoro,
P. O. Box 1,
LOLIONDO – NGORONGORO.

Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment
Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia
inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).

Maombi yatakayowasiIishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo
hili HAYATAFIKIRIWA.

DOWNLOAD PDF DOCUMENT HAPA

Tags:

Comments are closed.