RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI 15 za Kazi Manispaa ya Kigamboni July 2024

Filed in Ajira by on 19/07/2024

NAFASI 15 za Kazi Manispaa ya Kigamboni July 2024

NAFASI 15 za Kazi Manispaa ya Kigamboni July 2024

NAFASI 15 za Kazi Manispaa ya Kigamboni July 2024

NAFASI 15 za Kazi Manispaa ya Kigamboni July 2024,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni anawatangazia Watanzania wenye
sifa na nia ya kufanya kazi katika Manispaa ya Kigamboni kuomba nafasi za kazi ziliyotajwa hapo chini, baada ya kupokea kibali chenye Kumb. Na. FA.97/288/01/09 cha tarehe 25 Juni,
2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

✅DEREVA II – NAFASI 5

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari,
  • Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi,
  • Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari,
  • Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali,
  • Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari,
  • Kufanya usafi wa gari, na
  • Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na msimamizi wake.

SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa mwenye cheti cha kidato cha Nne (Form IV) na Leseni ya Daraja la “E” au “C” ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwakabmmoja bila kusababisha ajali na awe amehudhuria mafunzo ya Msingi ya uendeshaji Magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi ya Mishahara ya Serikali TGS B

✅WASAIDIZI WA KUMBUKUMBU II – NAFASI 10

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kuorodhesha barua zinazoingia masjala kwenye rejista (Incoming
    correspondence register)
  • Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya Taasisi kwenye rejista (Outgoing
    Correspondence register).
  • Kusambaza majalada kwa watendaji (action officers)
  • Kupokea majalada yanayorudi masjala toka kwa watendaji.
  • Kutafuta kumbukumbu/nyaraka /majalada yanayohitajika na Watendaji.
  • Kurudisha majalada kwenye kabati la majalada(Racks/filing cabinets) au mahali.pengene yanapohifadhiwa.
  • Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya Taasisi (file tracking).
  • Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na Msimamizi wake wa kazi.

SIFA ZA MWOMBAJI: –
Awe na Elimu ya kidato cha Nne (Form IV) au cha Sita (Form VI) aliehitimu
mafunzo ya Stashahada /Diploma (NTA Level 6) katika fani ya utunzaji wa
kumbukumbu kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, wenye ujuzi wa kompyuta.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi ya Mishahara ya Serikali TGS C

MASHARTI KWA UJUMLA KWA WAOMBAJI:

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini.
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuaninisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu
    walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
  • Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anuani inayotumika, namba ya simu za kuaminika, anuani ya barua pepe (E-mail Address) pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
  • Maombi yote yaambatane na Vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Mtihani wa Kidato cha IV au VI kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika
  • Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa
  • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTVET) na taarifa ya uhakiki iambatishwe kwenye maombi.
  • Testimonials, Provisional Results, Statement of results hati ya matokeo ya kidato cha nne na sita (form IV and form VI result slips) HAVITAKUBALIWA.
  • Uwasilishwaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
  • Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kungilia kazi kwa waajiri wao na waajiri wajiridhishe ipasavyo.
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.

Mwisho wa kupokea maombi ya kazi ni tarehe 27.07.2024.

Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa ajira
(Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo https://portal.ajira.go.tz/, aidha hakuna maombi yatakayopokelewa kwa njia tofauti na iliyotajwaMaombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili
HAYATAFIKIRIWA.

MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliosainishwa
pamoja na vyeti vya Elimu. Anuani ya barua hiyoielekezwe kwa: –
Mkurugenzi wa Manispaa,
Halmashauri ya Manispaa Kigamboni,
S.L.P. 36009,
Kigamboni – Dar Es Salaam.

DONWLOAD PDF DOCUMENT

Tags:

Comments are closed.