NAFASI 17 za Kazi Wilaya ya Morogoro July 16-2024
NAFASI 17 za Kazi Wilaya ya Morogoro July 16-2024
NAFASI 17 za Kazi Wilaya ya Morogoro July 16-2024,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro amepokea kibali cha Ajira chenye Kumb. Na. FA.97/288/01/09 cha tarehe 25/06/2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA MOROGORO 16-07-2024
Hivyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro anatangaza nafasi za kazi na anakaribisha maombi kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi hizo kama ifuatavyo:-
✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – NAFASI 02
MAJUKUMU YA KAZI YA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II
- Kuorodhesha barua zinazoingia Masijala kwenye regista (incoming correspondence register)
- Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya Taasisi (outgoing correspondence register)
- Kusambaza majalada kwa Watendaji (action officers)
- Kupokea majalada kwa Watendaji (action officers)
- Kupokea majalada yanayorudi masijala toka kwa Watendaji,
- Kurudisha majalada kwenye shabaka/kabati la majalada (racks/filling cabinets) au
mahali pengine yanapohifadhiwa, - Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya Taasisi (file tracking)
SIFA ZA MWOMBAJI
Mwombaji awe na Cheti cha Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI) aliyehitimu Stashahada (NTA level 6) katika fani ya Masijala kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali,
mwenye ujuzi wa Kompyuta.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia viwango vya mishahara ya Serikali – TGS C
✅DEREVA DARAJA II – NAFASI 05
MAJUKUMU YA KAZI YA NAFASI ZA DEREVA
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;
- Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi;
- Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari;
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali;
- Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari;
SIFA ZA MWOMBAJI
Mwombaji awe na Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) na Leseni ya Daraja E au C ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali.
Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo
kingine kinachotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia viwango vya mishahara ya Serikali – TGS B
✅MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA III – NAFASI 10
MAJUKUMU YA KAZI YA NAFASI ZA MTENDAJI WA KIJIJI
- Afisa Masuhuli na mtendaji mkuu wa serikali ya kijiji;
- Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao, kuwa mlinzi wa amani na msimamizi wa utawala bora katika kijiji;
- Kuratibu na kusimamia upangaji wa mipango ya maendeleo ya kijiji;
- Katibu wa mikutano na kamati zote za Halmashauri ya kijiji;
- Kutafsiri na Kusimamia Sera, Sheria na Taratibu;
- Kuandaa taarifa ya utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali;
- Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za kijiji;
- Mwenyekiti wa kikao cha wataalam waliopo katika kijiji;
- Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi;
- Kusimamia utungaji wa Sheria Ndogo za kijiji; na
- Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.
SIFA ZA MWOMBAJI
Mwombaji awe na Cheti cha kidato cha Nne (IV) au Sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo Cha Serikali za Mitaa au
Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali – TGS B
MASHARTI YA JUMLA
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45
- Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (Detail Curriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya
Barua Pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika. - Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma wapitishe barua zao za maombi
yanafasi ya kazi kwa waajiri wao. - Maombi yote yaambatane na nakala ya vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa
na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne/Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Diploma/Certificates, – Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, – Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma. - “Testmonial“, ‘‘Provisional Results“, “Statement of results“, hati ya matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
HAVITAKUBALIWA. - Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 29 Julai, 2024.
MUHIMU: Kumbuka kuambatanisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa na ielekezwe kwa anuani ya;-
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro,
S.L.P 1880,
MOROGORO
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).
Maombi yatakayowasiIishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili hayata shughulikiwa.
DONWLOAD PDF DOCUMENT
POST: MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – 2 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro More Details |
2024-07-29 Login to Apply |
POST: MTENDAJI WA KIJIJI III – 10 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro More Details |
2024-07-29 Login to Apply |
POST: DEREVA DARAJA II – 5 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro More Details |
2024-07-29 Login to Apply |