NAFASI 2 za Mtendaji wa Kijiji Wilaya ya Mbarali April 2024
NAFASI 2 za Mtendaji wa Kijiji Wilaya ya Mbarali April 2024
NAFASI 2 za Mtendaji wa Kijiji Wilaya ya Mbarali April 2024, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali anawatangazia nafasi ya kazi ya Mtendai wa Kijiji III. Nafasi hii inatokana na kibali cha Ajira Mbadala kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, chenye Kumb.Na FA.228/613/01/006 cha tarehe 07 Desemba 2023. Hivyo anapenda
kuwatangazia na kuwakaribisha Watanzania wote wenye sifa kutuma maombi kwa nafasi hizo kama ifuatavyo;-
MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA III – NAFASI (2)
SIFA ZA MWOMBAJI
- Awe amehitimu Kidato cha Nne (IV) au Sita (VI)
- Awe na Astashahada/ Cheti katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Rasilimali watu, Sheria, Maendeleo ya Jamii, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha aunSayansi ya Sanaa kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
KAZI NA MAJUKUMU YA MTENDAJI WA KIJIJI III
- Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji.
- Kusimamia Ulinzi na Usalama wa raia na mali zao, kuwa Mlinzi wa Amani na
- Msimamizi wa Utawala Bora katika Kijiji.
- Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaii wa Mipango ya Maendeleo ya Kijiji.
- Kuratibu Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji.
- Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na taratibu za uendeshaji wa Serikali ya Kijiji.
- Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umasikini na kuongeza uzalishaji mali.
- Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na Nyaraka za Kijiji.
NGAZI YA MSHAHARA
Mshahara atalipwa kwa kuzingatia Viwango vya Serikali TGS B.
MASHARTI YA JUMLA
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswabkuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwaajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya ajira katika utumishi wa umma.
- Waombaji wote waambatanishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa nabMwanasheria/Wakili.
- Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika Kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo. - Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (CV) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu
wenye kuaminika. - Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma,maelezo,nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha nne,Kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
- “Testimonials, Provisional Results, Statement of Result” na hati za matokeo kidato cha Nne na Sita (form IV na VI Result Slips) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma Nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimekaguliwa na kuthibitishwa na mamlaka husika (NECTA, NACTE na TCU).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwa kuomba isipokuwa kama wana Kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji kazi ambao tayari ni Waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia Maelezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa Tarehe 30 Novemba, 2010.
- Uwasilishaji taarifa za sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua Stahiki za Kisheria.
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI 04-04-2024 DOWNLOAD PDF
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 16/04/2024.
MUHIMU kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamoja na vyeti vya Elimu. Anuani ya barua hiyo ilekezwe kwa;
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya Mbarali,
S.L.P 237,
RUJEWA – MBARALI.
Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa Kielektroniki wa Ajira
(Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo: https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa
“Recruitment Portal”)
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioanishwa katika tangazo hili
HAYATAFIKIRIWA.
KUTUMA MAOMBI BONYEZA HAPA
POST: MTENDAJI WA KIJIJI III – 2 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali More Details |
2024-04-15 Login to Apply |
NAFASI 2 za Mtendaji wa Kijiji Wilaya ya Mbarali April 2024
Tags: NAFASI 2 za Mtendaji wa Kijiji Wilaya ya Mbarali April 2024