NAFASI 21 za Watendaji wa Vijiji Wilaya ya Tandahimba July 05-2024
NAFASI 21 za Watendaji wa Vijiji Wilaya ya Tandahimba July 05-2024
NAFASI 21 za Watendaji wa Vijiji Wilaya ya Tandahimba July 05-2024, Nafasi 21 za Kazi za Watendaji wa Vijiji Kutoka Halmashauri Wilaya ya Tandahimba July 05-2024, Ajira za Watendaji wa Vijiji Kutoka Halmashauri Wilaya ya Tandahimba July 05-2024.
Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba kupitia kibali cha ajira mbadala chenye Kumb. Na. FA. 228/613/01/C/032 cha tarehe 21 Mei, 2024 na kibali cha ajira mpya chenye kumb. Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25 Juni, 2024 chenye Kada ya Mtendaji wa Kijiji Daraja la III Ishirini na moja (21) kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Hivyo Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya
Tandahimba anatangaza nafasi za kazi na anakaribisha maombi kwa watanzania wote wenye sifa na kuleta maombi ya kazi kwa nafasi zilizoainishwa hapo chini,
✅MTENDAJI WA KIJIJI III – NAFASI 21
SIFA ZA KITAALUMA KWA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye elimu ya Kidato cha nne/Sita aliyehitimu mafunzo ya
Astashahada/Cheti (NTA LEVEL 5) katika fani zifuatazo; Utawala, Sheria,Elimu
ya Jamii, Usimamizi wa fedha, Maendeleo ya jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo au vyuo vingine vinavyoambuliwa na Serikali.
MAJUKUMU YA KAZI YA MTENDAJI WA KIJIJ III
- Kuwa Afisa masuhuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji
- Kusimamia Ulinzi na Usalama wa raia na mali zao, kuwa mlinzi wa amani na msimamizi wa utawala bora katika Kijiji
- Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya Kijiji
- Kuwa katibu wa mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji
- Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu
- Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo la kazi na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali
- Kuwa kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalam katika Kijiji
- Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Kijiji
- Kuwa Mwenyekiti wa kikao cha wataalamu katika Kijiji
- Kusimamia utungaji wa sheria ndogo za Kijiji
- Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi
- Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi ya Mshahara wa Serikali – TGS B1 kwa mwezi
MASHARTI YA JUMLA YA MAOMBAJI WA NAFASI ZA KAZI
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini;
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwaajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi waUmma
- Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (DetailCurriculum
Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya Barua Pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu
wa kuaminika. - Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia Sifa zakuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi yanafasi ya kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo. - Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detail C.V) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika; - Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia
sifa za kazi husika.
Postgraduate/Degree/Advanced
Diploma/Diploma/Certificates, – Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, – Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Professional Certificate from Respective Boards); - “Testmonial“, ‘‘Provisional Results“, “Statement of results“, hati ya matokeo yabKidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
HAVITAKUBALIWA. - Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 18/07/2024
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa: –
Mkurugenzi Mtendaji (W),
S.L.P O3,
TANDAHIMBA – MTWARA.
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira kupitia anwani
ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa (‘Recruitment Portal’)
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
POST: MTENDAJI WA KIJIJI III – 21 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba More Details |
2024-07-18 Login to Apply |
Tags: Ajira za Watendaji wa Vijiji Kutoka Halmashauri Wilaya ya Tandahimba July 05-2024., Nafasi 21 za Kazi za Watendaji wa Vijiji Kutoka Halmashauri Wilaya ya Tandahimba July 05-2024, NAFASI 21 za Watendaji wa Vijiji Wilaya ya Tandahimba July 05-2024