NAFASI za Kazi Kutoka Wilaya ya Momba 21-05-2024
NAFASI za Kazi Kutoka Wilaya ya Momba 21-05-2024
NAFASI za Kazi Kutoka Wilaya ya Momba 21-05-2024, Ajira Mpya kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Momba Leo May 2024, Nafasi za Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja La Ii Halmashauri ya Wilaya ya Momba Leo May 2024, TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA MOMBA 21-05-2024.
- NAFASI za Kazi Kutoka Ajiraportal May 2024
- NAFASI 3 za Mtendaji wa Kijiji Wilaya ya Kondoa May 2024
- MAJINA 49 ya Walioitwa Kwenye Usaili Wilaya Ya Kishapu 21-05-2024
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba alipokea kibali cha Ajira kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa barua yenye Kumb. Na. FA.228/613/01/B/015 ya tarehe 22 Aprili, 2024. Hivyo anawatangazia Watanzania wote wenye sifa kutuma maombi kwa nafasi zifuatazo;
1.0 MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II-NAFASI 1
SIFA ZA MWOMBAJI
- Mwombaji awe na Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) na mwenye Stashahada (Diploma) ya Uhazili au cheti cha NTA level 6 ya Uhazili.
•Awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 80 kwa dakika moja na kupata programu ya kompyuta za ofisi kama vile: word, Excel, powerpoint, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na serikali.
KAZI NA MAJUKUMU
- Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na siri.
- Kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa.
- Kutunza taarifa na kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine.
- Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi.
- Kupokea majalada na kusambaza kwa Maofisa walio katika Idara/Kitengo/Sehemu husika.
- Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika,
- Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali na Kuandaa orodha ya mahitaji vya vifaa vya ofisi.
MSHAHARA
Mshahara atalipwa kwa kuzingatia viwango vya Serikali TGS C1
MASHARTI YA JUMLA
- Waombaji wote wawe ni raia wa Tanzania wenye umri kuanzia miaka 18 na wasiozidi miaka 45.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira aina ya ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
- Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza Curriculum Vitae (CV) na anuani ya Barua Pepe yenye Anuani inayotumika, namba ya simu (E-mail address) pamoja na majina ya Wadhamini ( Referees) watatu wa kuaminika.
- Matokeo ya muda (provisional/Testimonials/ Statement of Results) havitakubaliwa.
- Kilichothibitishwa waambatanishe wote Waombaji Mwanasheria/Wakili, cheti cha kuzaliwa na
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi ya kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo.
- Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
- Maombi yote yaambatane
na na vyeti vya taaluma vilivyothibitishwa Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne, Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia zifa za kazi husika. - Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NACTEVET na NECTA).
- Uwasilishaji wa Taarifa na Sifa za kughushi, wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
- Barua ya maombi itatakiwa iandikwe kwa Kiswahili au Kingereza.
MUHIMU: kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya Elimu, aidha anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:
Mkurugenzi Mtendaji.
Halmashauri ya Wilaya ya Momba,
S.L.P 273,
MOMBA.
Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo: https://portal.ajira.go.tz/advert/index anuani hii pia inapatikana kwenye Tovuti ya Sekterarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa “Recruitment Portal”.
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 03 Juni, 2024.
CLICK HERE TO DONWLOAD PDF DOCUMENT
POST: MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – 1 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Momba More Details |
2024-06-03 Login to Apply |
Historia ya Halmashauri ya Wilaya ya Momba
Wilaya ya Momba, ni miongoni mwa wilaya mpya, ilianzishwa rasmi mwaka 2012 na Serikali kwa mujibu wa kifungu cha tano (5) sheria za Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya), sura namba 287 R.E 2012 na pamoja na sheria nyinginezo zinazohusika na uanzishwaji wa Wilaya ni pamoja na Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Sheria ya uanzishwaji wa mikoa na Wilaya sura namba 397 ya mwaka 2012, baada ya kugawanya kwa Wilaya ya Mbozi kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wakazi wa Wilaya ya Momba, kufuatia tangazo la Serikali (GN) Namba 73 la mwaka 2012 wilaya ya Momba ilitangazwa kuanzishwa rasmi pamoja na wilaya nyingine 18, hati rasmi ya uanzishwaji wa wilaya ya Momba na kuanza kutumika ilitolewa tarehe 23/12/2012.
Wilaya ya Momba inaundwa na halmashauri mbili , halmashauri ya Wilaya ya Momba na halmashauri ya Mji wa Tunduma, ambazo kwa pamoja zina tarafa 4, halmashauri ya wilaya ya Momba ikiwa na tarafa 3 na jimbo moja la uchaguzi na halmashauri ya Wilaya ya mji wa Tunduma ikiwa na tarafa 1 na jimbo moja la uchaguzi.
Wilaya ya Momba inapatikana Magharibi mwa Mkoa mpya wa Songwe, kati ya Latitudo 80 10” Kusini na 90 15”kusini mwa mstari wa Equator, Longitudo 320 5’Mashariki na 320 45” Mashariki mwa mstari wa Greenwich ya Meridian. Wilaya inapakana na Mkoa wa Rukwa na Nchi ya Zambia upande wa Magharibi, Upande wa Mashariki inapakana na Wilaya ya Mbozi, Upande wa Kaskazini inapatikana na Wilaya ya Chunya, na kusini inapakana na Wilaya ya Ileje.
Tags: Ajira Mpya kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Momba Leo May 2024, NAFASI za Kazi Kutoka Wilaya ya Momba 21-05-2024, Nafasi za Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja La Ii Halmashauri ya Wilaya ya Momba Leo May 2024, TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA MOMBA 21-05-2024.