RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI za Kazi Manispaa ya Ubungo August 01-2024

Filed in Ajira by on 01/08/2024

NAFASI za Kazi Manispaa ya Ubungo August 01-2024

NAFASI za Kazi Manispaa ya Ubungo August 01-2024

NAFASI za Kazi Manispaa ya Ubungo August 01-2024

NAFASI za Kazi Manispaa ya Ubungo August 01-2024, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo amepokea Kibali cha Ajira Mbadala kutoka kwa Katibu Mkuu OR – Utumishi chenye Kumb.Na. FA. 228/613/01/D/040 ya tarehe 09.07.2024.

Hivyo anapenda kuwatangazia Watanzania wote wenye sifa kutuma maombi kwa kada moja (1) kama ilivyoainishwa kwa kuzingatia sifa tajwa hapo chini: –

MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II – NAFASI 1

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kuorodhesha barua zinzoingia masjala kwenye rejista (incoming correspondence
    register);
  • Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya taasisi kwenye rejista (outgoing correspondence register);
  • Kusambaza majalada kwa watendaji (action officers);
  • Kupokea majalada yanayorudi masijala toka kwa watendaji;
  • Kutafuta kumbukumbu/ nyaraka/majalada yanayohitajika na watendaji;
  • Kurudisha majalada kwenye shubaka/kabati la majalada
    ( racks / filling cabinets) au mahali pengine yanapohifadhiwa
  • Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya Taasisi (file tracking)

SIFA ZA MWOMBAJI
Awe Muhitimu wa Kidato cha Nne au Sita mwenye Stashahada au NTA level 6 ya Utunzaji wa Kumbukumbu kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali, mwenye ujuzi wa Kompyuta.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za Mishahara ya Serikali -TGS C.

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri kuanzia miaka 18 – 45
  • Waombaji wote waambatanishe nakala ya cheti cha kuzaliwa.
  • Barua ya muombaji ioneshe anuani anayotumia kwasasa pamoja na namba ya simu
    ikiambatana na:-
  • Nakala za vyeti vya taaluma.
  • Nakala ya vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kidato cha nne, sita na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa na kazi husika.
  • Maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed CV) yenye anuani na namba za simu zinazopatikana na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
  • Picha mbili (2) za “Passport Size” za hivi karibuni.
  • Kitambulisho cha Taifa au namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA)
  • Waombaji waliowahi kupatikana na kosa la jinai hawatafikiriwa
  • “Testmonies”, “Provisional Result”, “Statement of Results” hati ya matokeo ya Kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULT SLIPS
    HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
    kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  • Waombaji waliostaafishwa/ kuachishwa kazi katika
    Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama ana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi, wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
  • Waombaji wenye sifa zaidi ya zilizotajwa hapo juu maombi yao hayatafikiriwa.

Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 09 Agosti, 2024.

MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
Mkurugenzi wa Manispaa,
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo,
S.L.P 55068,
DAR ES SALAAM.

Maombi yote yatumwe kwenye Mfumo wa Kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa “Recruitment Portal”.

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioanishwa katika tangazo hili
HAYATAFIKIRIWA.

DOWNLOAD PDF DOCUMENT HAPA

Tags:

Comments are closed.